Watumiaji wa huduma za mawasiliano wanashauriwa kujihadhari dhidi ya utapeli kwenye
mitandao ya simu za mkononi kama ifuatavyo:
1. Usiweke taarifa nyingi za binafsi na za undani kwenye mitandao ya jamii.
2. Neno la siri ni muhimu sana katika kutunza anwani yako ya barua pepe au akaunti yako ya
mtandao wa jamii. Chagua neno la siri ambalo linachanganya maneno na tarakimu.
3. Ukisaidiwa kuanzisha mtandao wa kijamii hakikisha unabadilisha neno la siri baada ya kukabidhiwa.
4. Badilisha neno la siri mara kwa mara. Muda unaopendekezwa ni angalau kila baada ya siku
90.
5. Usirudie kutumia neno la siri ulilowahi kulitumia.
6. Iwapo una anwani ya barua pepe au akaunti ya mtandao wa jamii zaidi ya moja, tumia
maneno ya siri tofauti kwa kila moja.
7. Usimpe mtu yeyoye, hata wa karibu, neno la siri unalotumia kwenye anwani au akaunti
zako.
8. Usiandike mahali popote neno la siri unalotumia. Tumia maneno ambayo ni rahisi
wewe kukumbuka lakini magumu kwa mtu mwingine kukisia.