Watu wengi wanaotumia mitandao kama Instagram ni wapenzi wa pichaz, hasa vijana yani time zote utakuta tu wanapost picha zao wakishare na marafiki zao basi inakuwa poa.
Sasa sio kila sehemu unaruhusiwa kuingia na selfie stick kwa ajili ya kujiselfie, Majumba ya Maonesho ya sanaa Uingereza wamepiga marufuku mtu yoyote kuingia na selfie stick ndani ya majumba hayo.
Uamuzi wa kuzuia mtu yoyote kutumia selfie stick unatokana na mapendekezo yaliyotolewa na watu wanaosimamia Nyumba za Sanaa za Maonesho.. wanasema watu wanaoingia na selfie stick na kupiga picha wanawazuia watu wengine kuenjoy kuangalia picha na vitu mbalimbali vilivyomo ndani ya majumba hayo, vilevile sio salama sana kwa picha ambazo zinaning’inizwa kwenye majumba hayo.
Uingereza sio wa kwanza kuzuia selfie stick, Marekani pia walitangaza kuzuia matumizi ya vifaa hivyo kwenye Majumba ya Makumbusho.. Arsenal ilizuia mtu yoyote kuingia uwanja wa Emirates wakati wa mechi kwa kuwa kifaa hicho wanakichukulia kama silaha nyingine tu kwa hiyo ni hatari kama mtu akiingia nayo uwanjani.
Manchester United nao walizuia, Tottenham Hotspurs nao walitangaza kwamba watazuia mtu yoyote kuingia kwenye Uwanja wao wa White Hart Lane na selfie stick.
Cookie Monster + @metmuseum‘s Washington Crossing the Delaware via @mashable#museumselfiepic.twitter.com/tDCfncNnv4
— Fraser McDonald (@FraserMcDonald) March 5, 2015
Korea Kusini walienda mbali zaidi, mpango wao ilikuwa ni kuzuia kabisa selfie stick..
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook