Staa wa China maarufu zaidi kwa kwenda live na kutangaza bidhaa mbalimbali, yaani live streamer amepigwa faini ya dola Milioni 210 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 484 kwa kukwepa kodi.
Huang Wei maarufu kama Viya, ni staa wa mitandao ya kijamii mwenye mamilioni ya followers. Amekuwa akitumia akaunti yake kuuza bidhaa mbalimbali.
Mamlaka huko Hangzhou zimemshutumu kuficha utajiri wake pamoja na makosa mengine ya kifedha kati ya mwaka 2019 na 2020.
Kwenye post aliyoweka kwenye akaunti yake ya Weibo ameomba radhi na kukiri makosa hayo. Viya mwenye miaka 36 anafahamika kama malkia wa live-streaming nchini China na amekuwa akizipigia debe biashara nyingi kwenye jukwaa la Taobao.
Umaarufu wake umemfanya atajwe kwenye orodha ya mwaka huu ya Time ya watu 100 wenye ushawishi duniani. Akaunti yake ya Weibo iliyokuwa na followers milioni 18 haipo tena.
China ina tasnia kubwa zaidi ya live-streaming ambapo kuna zaidi ya vloggers milioni 400.