Siku zote mchezo wa soka unahitajika uwe na nidhamu, mchezaji soka unatakiwa kuzingatia vitu kadhaa ili ulinde kipaji chako na kuendelea kucheza soka. Ni maswali ambayo wengi tunajiuliza kwa nini watu wanavuta sigara wakati ni hatari kwa afya zao, basi kwa wanamichezo sigara haishauriwi kutumia hata siku moja. Hii ni list ya mastaa 10 wa soka wanaovuta sigara.
10- Wojciech Szczesny kwa sasa yupo katika klabu ya AS Roma ya Italia ila kitendo chake cha kuvuta sigara kilimfanya apoteze namba katika kikosi cha Arsenal kitu kilichopelekea kutolewa kwa mkopo katika klabu ya AS Roma. Wojciech Szczesny alipigwa faini ya pound 20,000 kwa kufanya kosa hilo.
9- Wesley Sneijder kiungo wa kimataifa wa Kiholanzi ambaye amewahi kufanya vizuri katika vilabu kadhaa ikiwemo Inter Milan ya Italia, yupo katika list ya wavutaji sigara. Wesley Sneijder ni moja kati ya wachezaji wa timu ya taifa ya Uholanzi waliosaidi timu yao kufika fainali ya Kombe la Dunia 2010 na baadae wakapoteza mchezo huo kwa goli 1-0 dhidi ya Hispania.
8- Lionel Messi aliwahi kuonekana akivuta sigara katika mapumziko ya msimu lakini huenda akawa anavuta kwa siri. Anatajwa kuwa mtaratibu katika mambo yake. Kwa sasa Lionel Messi anauguza jeraha katika mguu wake lakini amelazimika kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki nane.
7- Fabien Barthez ni golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa kuna wakati Paul Scholes aliwahi kusema Fabien Barthez na Laurent Blanc hawawezi kuanza kufanya mazoezi bila kuvuta sigara kwa sasa Barthez amestaafu soka.
6- Wayne Rooney mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza na nahodha wa klabu ya Manchester United. Rooney aliwahi kupigwa picha akiwa anavuta sigara wakati yupo likizo ya mapumziko ya mwisho wa msimu.
5- Mario Balotelli anatajwa kuwa ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu lakini tabia yake ya utukutu imekuwa ikimpunguzia baadhi ya sifa njema. Mario Balotelli anatajwa kuwa mvutaji wa sigara mzuri na mara kadhaa amewahi kupigwa picha na waandishi wa habari akivuta sigara.
4- David Ginola huenda jina lake likawa geni masikioni mwako ila huyu ni staa wa soka wa Ufaransa aliyewahi kutamba katika vilabu vya Newcastle na Tottenham Spurs anatajwa kuwa alikuwa anavuta sigara hata ndani ya basi la timu na wachezaji wenzake wakiwemo bila kujali kuwa ataathiri afya za wengine.
3- Ashley Cole ni beki wa zamani wa klabu ya Chelsea na Arsenal kwa sasa anaichezea klabu ya AS Roma ya Italia, beki huyo wa pembeni ni mvutaji wa sigara mkubwa na moja kati ya kitu kilichofanya apoteze namba katika kikosi cha Jose Mourinho ni tabia yake ya kupenda kuvuta sigara kitu ambacho Mourinho hakipendi.
2- Dimitar Berbatov ni mshambuliaji wa kimataifa wa Bulgaria ambaye alishindwa kutamba katika klabu ya Manchester United licha ya kuwa alikuwa tumaini kubwa kwa Ferguson na mashabiki wa Man United Berbatov ni mvutaji mahiri wa sigara pamoja na uongozi wa timu nyingi za Uingereza kutopenda tabia hiyo ya uvutaji wa sigara. Kuna wakati aliwahi kuulizwa kwa nini anavuta sigara jibu lake alisema “sivuti sigara huwa najifanyisha kama navuta sigara ili kujiweka sawa”
1- Jack Wilshere amewahi kukamatwa akivuta sigara katika klabu za usiku na katika bwawa la kuogelea Las Vegas Marekani na kuna wakati alikutwa akivuta shisha baada ya kuulizwa kuhusiana na tabia hiyo Wilshere alijibu ” mimi ni mdogo na nitajifunza kitu kupitia hili”
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.