Mkataba mnono walioupata klabu ya Stand United ya Shinyanga kutoka katika kampuni ya uchimbaji madini inaonekana kuzidi kuutumia vizuri kwa kuongeza nguvu katika kikosi chake kwani imewasajili wachezaji nyota wawili.
Klabu hiyo imethibitisha kumsajili kiungo wa zamani wa Simba Amri Kiemba na kiungo wa zamani wa Dar Es Salaam Young African, Hassan Dilunga, msemaji wa Stand United Deokaji Makomba amethibitisha kusajiliwa kwa wachezaji hao kwa mkataba wa mwaka mmoja kila mmoja.
“Kiemba anatarajia kurejea hapa Shinyanga leo kuungana na wenzake kwa ajili ya kwenda Kahama ambako tutaweka kambi, Dilunga suala lake limemalizika naye amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Stand chama la wana”>>> Deokaji Makomba
Kiemba amewahi kuichezea klabu ya Simba kabla ya kutimkia Azam FC na sasa Stand United ya Shinyanga huku Dilunga aliwahi pia kujiunga na Dar Es Salaam Young African akitokea JKT Ruvu ya Kibaha Pwani.
CHANZO CHA HII STORY>>>SALEH JEMBE
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos