Bado zile stori za Raheem Sterling kuhama Liverpool na kujiunga na Manchester City pamoja na kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Brendan Rodgers zinazidi kuchukua headlines. Wakala wa winga huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye asili ya Jamaica Aidy Ward amefunguka na kueleza kuwa aliyesababisha Raheem Sterling ahame Liverpool ni Brendan Rodgers.
“Raheem angeweza kubakia Liverpool, nafikiri kwangu mimi nilikuwa nimeshazungumza na Raheem na angesaini mkataba mpya, mwezi December nilizungumza na Liverpool kuhusu Raheem kusaini mkataba mpya kama tu vipengele vya mkataba wake vingewekwa wazi kama mikataba mingine ilivyo” >>> Aidy Ward
“Lakini katika mkutano na waandishi wa habari Rodgers alithibitisha kuwa Raheem atasaini licha ya kuwa hatukuwa tumefikia makubaliano yoyote, kwa nini alifanya vile? nilijua Rodgers na Liverpool walikuwa wanajua kinachoendelea, lakini kwa sasa angeweza kuwa mchezaji wa Liverpool lakini yupo Man City ni sehemu nzuri kwake”>>> Aidy Ward
Kuondoka kwa Raheem Sterling ndani ya Liverpool kuliweka headlines nyingi katika vyombo vya habari vya Uingereza hususani ukilinganisha na dau la usajili la pound milioni 49 walilotoa Man City ili wapate saini ya nyota huyo kinda wa kiingereza.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.