Ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Stella Manyanya ambae leo ametangaza kuhusu kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Maswala ya Walaji ambae atapangiwa kazi nyingine.
Namnukuu akisema “Wizara yetu imedhamiria kuhakikisha kwamba tunaondoa malalamiko yote ambayo yamekua yakijitokeza kwenye Taasisi zetu ambazo zinahusika aidha kufatilia viwango au huduma za Walaji kwa ujumla”
“Hatutavumilia kuona mtu yeyote, Taasisi au kikundi cha watu kikilalamikiwa alafu sisi tukaangalia, kimsingi Mtumishi ambae anahusika na shughuli hizo hatakiwi kulalamikiwa… na kwa misingi hiyo narudia kumuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji”
“Tukianza na FCC Mkurugenzi anaehusika na maswala ya Walaji aondolewe mara moja atapangiwa shughuli nyingine, vilevile kuna baadhi ya Watumishi walikua kwenye Taasisi hiyo ambao kumekua na malalamiko ya rushwa na kutokutoa huduma kwa wakati hao tunaanza nao wanaondoka”
“Tutaendelea kufanya hivyohivyo katika Taasisi nyingine kama TBS na yenyewe hivyohivyo kuna baadhi ya mambo ambayo hayajakaa vizuri na maeneo mengine, sasa hivi ni kipindi cha HAPA KAZI TU na kila mtu ahakikishe anatimiza wajibu wake ” – Naibu Waziri Stella Manyanya
“Kiongozi ni kusikiliza watu, Serikali mnaficha nini? – Hussein Bashe… bonyeza play hapa chini kumtazama