October 6 2016 Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mbeya Rehema Madusa amekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia mpango wa serikali baada ya kutoa zuio la ukataji miti inayotumika katika shughuli za kibiashara ikiwemo uchomaji mkaa katika wilaya yake huku akiagiza kusimamishwa kazi kwa afisa wa TFS kwa tuhuma za kuhusika na usafirishaji wa misitu.
DC Rehema amesema…>>>’Kutokana na uvunaji holela wa mazao ya misitu katika Wilaya ya Chunya pamoja na uvujaji wa mapato ya mazao ya misitu nasitisha zoezi la uvunaji wa mkaa, mbao na magogo katika wilaya yetu ya Chunya kuanzia November 1 2016‘
‘Mamlaka za misitu itatakiwa kutotoa leseni za mazao tajwa kuanzia October 1 2016 pia itatakiwa kuwakamata wavunaji wote wasio na vibali‘ –DC Rehema Madusa
‘Mwisho wa kusafirisha mazao yote yaliyohakikiwa ni October 30 2016, na yeyote atakayepatikana baada ya tarehe tajwa akisafirisha mazao hayo atashughulikiwa kisheria na mamlaka husika‘ –DC Rehema Madusa
‘Ninamwagiza mkurugenzi mkuu wa TFS kumsimamisha ofisa wa TFS wakati tunajipanga kuchukua hatua za kisheria baada ya kubainika na tuhuma za kuwasaidia wavunaji wasio na vibali halali kusafirisha mazao ya misitu‘ –DC Rehema Madusa
Unaweza kuendelea kumsikiliza DC Rehema kwenye hii video hapa chini…
ULIMIS MAAMUZI YA SERIKALI BAADA YA KUONA ILE VIDEO YA WALIMU WAKIMPIGA MWANAFUNZI