MTANZANIA
Serikali imetangaza rasmi kuanza mpango wa kutengeneza barabara zitakazotumiwa kwa kulipia kutoka Dar es salaam hadi Mkoani Morogoro.
Hatua hiyo ya Serikali imekuja wakati foleni za barabarani zikizidi kuongezeka kwa kasi katika jiji la Dar es salam jambo ambalo limekua likilalamikiwa na wananchi.
Waziri wa Ujenzi John Magufuli alisema mradi huo utakua wa awamu mbili ambapo ya kwanza itaanza Dar hadi Chalinze na nyingine Chalinze hadi Morogoro.
Alisema sababu ya kuchukua uamuzi huo ambao umekua ukichutumiwa na nchi nyingine zilizoendelea duniani imechangiwa na tathmini iliyotolewa ikionyesha kwa siku zinapita gari 56,000 katika barabara ya Morogoro.
“Kwa hali hii takwimu zinaonyesha kati ya mwaka 2015 hadi2016 magari yatakuwa yakishikana kutokana na msongamano,ndipo tukafikiria utaratibu huu ambao utasaidia watu mbalimbali wenye uwezo wa kulipia ili wasikae katika foleni,”alisema Magufuli.
Alisema faida zitokanazo na utumiaji wa njia hizo utasaidia kuokoa muda na kupunguza ajali barabarani na gharama kidogo za mafuta kutokana na kuwa na mwendo kasi wa kilomita 120 kwa saa.
MWANANCHI
Kambi ya upinzani Bungeni jana limsulubu Waziri wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe ikieleza kuwa Wizara yake iliingia mkataba wa wa mradi wa treni za kisasa kutoka stesheni .ya Dar es salaam hadi Pugu kupitia uwanja wa ndege wa JNIA bila kufuata taratibu.
Kambi hiyo ilieleza Bungeni kuwa mkataba huo ulisainiwa baina ya mmliliki wa kampuni ya M/S Shomoja Robert Shumake na Sirika la Reli Tanzania huku Waziri huyo akishuhudia.
Msemaji mkuu wa kambi hiyo ya upinzani Pauline Gekul alisema taratib hazikufuata na kuwa haieleweki ni lini Serikali,Wakala au Wizara ya uchukuzi ilitangaza Zabuni ya mradi wa treni kutoka stesheni hadi pugu kupitia JNIA.
Alisema ni wazi kwa kifupi Mwakyembe na Wizara yake walikiuka vifungu vya sheria ya PPP na alivitaja vifungu hivyo kuwa ni 4(1) na(2) vinavyomtaka Waziri kutangaza katika Gazeti la Serikali miradi mbalimbali inayotegemewa kufanywa na sekta ya umma kwa ubia na sekta binafsi.
MWANANCHI
Bohari kuu ya Dawa MSD imeanza kusambaza dawa katika hospitali mbalimbali nchini ba ada ya kupokea kiasi cha bilioni20 ambazo ni sehemu ya malipo ya deni linaloidai Serikali
Kaimu Mkurugenzi mkuu wa MSD Cosmas Mwaifani alisema fedha hizo zitapunguza kwa kiasi kidogo deni hilo ingawa alisema bohari hiyo haijawahi kukataa kutoa dawa katika hospitali yoyote.
“Kama wana fedha za kutosha hilo kwetu si tatizo kwa sababu dawa tunazo,wakifuata masharti ya ununuzi sisi tunawapa dawa,”alisema.
Alisema fedha walizopewa tayari zimeshaingizwa katika mzunguko wa ununuzi wa dawa kwa baadhi ya hospitali kwa kufuata vipaumbele na kuhusu shehena ya dawa kukwama bandarini ni kawaida kwa mizigo kukwama kutokana na mchakato mrefu wa utoaji mizigo ambao unahusisha sehemu nyingi za ukaguzi na uthibiti.
Kauli ya Mwaifani imekuja wakati kukiwa na taarifa kutoka hospitali mbalimbali hasa za Serikali ambao watendaji wake wakuu wamedai kwamba hawajapokea dawa toka MSD badala yake wametumia njia mbadala ikiwa ni pamoja na kutumia fedha wanazokusanya kutoka kwa wagonjwa kwa ajili ya kununulia dawa za wa dharura.
MWANANCHI
Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto imeagizwa kuanza utekelezaji wake wa faini za papo kwa papo ya shilingi 50,000 kwa watakaobainika kuchafua mazingira kwa makusudi.
Agizo hilo lilitolewa jana na mkuu wa Wilaya ya Lushoto Magid Mwanga wakati wa kongamano la kuhamasisha usafi na utunzaji wa mazingira lililoandaliwa na Shirika la wanawake la utunzaji mazingira YWCA kupitia mradi wa wajibika.
Alisema pamoja na jitihada zilizochukuliwa na ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi bado kunabaadhiya watu wanakwamishajitihada hizo makusudi.
“Umefikia wakati sasa sheria lazima zianze kutumika,watu wanachafua mazingira kama vile hakuna sheria na hakuna hatua yoyote inayotolewa,nadhani sasa ni wakati wake tutahakikisha faii hii inakuwa maini na inatumika kwa wale wote wanaovunja sheria hizo”alisema Mwanga.
JAMBOLEO
Vibanda zaidi ya 200 vimeteketea kwa moto katika soko maarufu la kuuza vinyago na madini ya aina mbalimbali katika eneo la Fire jijini Arusha na kuleta hasara ya zaidi ya bilioni8.
Moto huo ambao ulitokea juzi usiku huku kikosi cha zima moto kikilaumiwa kufumbia macho suala hilo hadi ukateketeka idadi hiyo ya vibanda,Kaimu mkuu wa Mkoa Magesa Mulongo amesema askari hao watawajibishwa.
Mulongo alisemapamoja an soko hilo kuwa karibu na makao makuu ya ya ofisi za zimamoto lakini askari hao walishindwa kuokoa mali za Wafanyabiashara hao na kwamba hatua za inidhamu zinachukuliwa dhidi yao.
“Nitawaajibisha askari wa zimamoto kwa sababu hii si sawa kabisa,kutoka hapa na ofisini kwao hakuna umbali wowote,iweje washindwe kudhibiti huu moto,lazima wajieleze na hata kushtakiwa”alisema Mulungo.
Mashuhuda wa ajali hiyo walisema kama si uzembe wa askari hao baadhi ya mali za wafanyabiashara hao zingeokolewa lakini askari hao walifika eneo la tukio na kushindwa kufanya kazi kwa kuwa walikua wamelewa.
JAMBOLEO
Jamaa mmoja Evgvin Sapeev mwenye miaka38 nchini urusi ametoa kali baada ya kujikata sehemu zake za siri ilimradi ageuke kuwa mwanamke.
Kikubwa kilichomfanya jamaa huyo ambaye ni msanii wa filamu kujikata kiungo hicho muhimu cha uzazi ni kwamba alitamani siku moja kugeuka kuwa mwanamke kutokana na kuvutiwa na wanawake.
Mwanaume huyo alionekana akitoka nje ya nyumba yake huku damu zikimtoka kutokana na kitendo hicho ambacho alikifanya mwenyewe na watu kuamua kumkimbiza hospitali baada ya hali yake kuwa mbaya.
Madaktari walijaribu kumsoma ili kurejesha maumbile yake lakini hawakufanikiwa na alivuja damu nyingi ambazo zilihatarisha maisha yake kwai angeweza kufariki.
Baadhi ya majirani zake walimkosoa msanii huyo kujikata sehemu za siri badala ya kwenda hospitali kufanyiwa upasuaji kwa njia iliyo salama.
NIPASHE
Zaidi ya Mameya50,Maofisa mipango miji na wataalam mbalimbali kutoka majiji 25 duniani wanakutana jijini Dar es salaam katka mkutano wenye kauli mbiu ‘Fikiri nje ya mipaka yako’ na kubadilishana uzoefu katika katika kusimamia ukuaji haraka wa miji kupitia mipango miji.
Mkutano huo unajulikana kama Global Lab, umeandaliwa kwa ushirikiano a benki ya dunia na Jiji la Dar es salaam.
Mkurugenzi mkazi wa benki ya dunia Philippe Dongie alisema jiji la Dar ni miongoni mwa majiji yanayokua kwa kazi duniani na kwamba ukuaji huo unapaswa kuwekewa mazingira rafiki ya ukusanyaji kodi,kurekebisha mipangilio ya utawala ili kuwezesha upangaji wa miji.
Alisema inalenga kuhakikisha miji ufanisi wa mipango miji kwa manufaa ya wakati wake kwenye sekta za uchumi,shughuki za jamii na mazingira yanayowazunguka.
Alisema katika mkuttano huo washiriki watapata fursa ya ujadii namna ya kuhakikisha mipango miji na majiji unakua endelevu kwa kuhakikisha huduma muhimu kama usafiri na miundombinu ,makazi,maji vinapatikana.
HABARILEO
Juhudi za Serikali za kukabiliana na foleni katikati ya jiji la Dar es salaam zimeendelea kushika kasi ambapo siku moja baada ya kupokelewa kwa kivuko cha Mv Dar,jana imetangaza mpango wa kujenga barabara itakayopita juu ya maji kutoka ufukwe wa Coco hadi hospitali ya Aga Khani ,Upanga na tayari makubaliano hayo yamefikiwa kati ya Serikali na Korea kusini.
Barabara hiyo itakua na urefu wa km7.1 huku daraja litakalounganisha barabara hiyo kupita juu ya bahari litakua na urefu wa km1.2 nalitakua na njia nne za waenda kwa miguu.
Waziri wa ujenzi John Magufuli alisema daraja la Salender lilijengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japanna haliwezi kubomolewa kwa kuwa Serikali ina historia kubwa na Japan hivyo si jambo la busara kubomoa kwa kuwa linapitisha magari 51,000 kwa siku.
Alisema barabara hiyo itakua na uwezo wa kupitisha magari61,000 kwa siku hivyo hupunguza msongamano mkubwa wa magari na ndilo lengo la Serikali na tayari michoro kwa ajili ya ujenzi huo umekamilika na ujenzi utaanza ndani ya miezi24.
HABARILEO
Serikali imesema asilimia80 ya madini ya Tanzanite yanayochimbwa nchini pekee katika mji wa Mererani yanauzwa nje ya nchi kwa njia za panya.
Kamishna wa Madini wa Wizara ya Nishati Paul Masanja alisema asilimia 20 tu ya madini hayondio yanauzwa kihalali hali inayosababisha Serikali kupata hasara kubwa kwa Taifa, licha ya ukweli kwamba madini hayo yanapatikana Tanzania tu.
Alisema kiasi hicho cha madini kilichouzwa kihalali nje ya nchi ni dola za Marekani milioni38 sawa na bilioni64.6 kwa mwaka na imesikitishwa kuona nchi jirani za Kenya inauza madini ya Tanzanite nje kwa kiasi cha dola za Marekani milioni100 sawa na bilioni170 hali inayofanya wafanyabiashara wote wa madini kutokuwa waaminifu katika biashara zao.
Alisema si kwamba Serikali haijui kuwa madini ya Tanzanite yanapitishwa kimagendo kwa njia ya panya mipakani na viwanja vya ndege,bali imejipanga kupambana na hali hiyo kikamilifu na wahusika wote watatiwa ndani mara muda utakapotimia
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook