Omayra Sanchez alikuwa ni mtoto wa kike, alikufa na umri wa miaka 13, mwaka 1985 katika janga la volkano huko Colombia katika kijiji cha Armero.
Baada ya volkano kulipuka na kuharibu miundombinu ya kijiji hicho, Omayra alikwama katika harakati za kujiokoa kutoroka tukio hilo.
Alikwama sehemu ambayo ilikuwa na dimbwi la maji, nje ya nyumba yao baada ya nyumba hiyo kuharibika na kudondoka kwenye dimbwi hilo.
Baada ya kukwama kutokana na hali duni ya vifaa vya uokoaji kwa wakati ule ilikuwa ni vigumu kuweza kumnasua mtoto huyo ambaye miguu yake ilikuwa umekandamizwa na ukuta pamoja na mbao za nyumba .
Zoezi la uokoaji wa mtoto huyo lilitumia siku tatu ,pasipo mafanikio mpaka mauti ya lipo mkuta.
Mpiga picha maarufu Frank Fourmer alikuwa kwenye tukio ndio aliye piga picha maarufu ya mtoto huyo muda mchache kabla ya kukata kauli ya mwisho.Picha ambayo ilizua gumzo pande zote duniani.
Mpiga picha alisimulia kwamba ilikuwa ni tukio la kusikitisha kuwahi kushuhudia baada ya kuona hisia za mtoto yule pale alipokuwa akiangaika na kulia .
Omayra katika saa 60 za mateso yake alionekana katika hali tofauti tofauti kabla ya umauti mkuta, mara nyingi alionekana akifurahi kuimba na kucheka akiamini ataokolewa kwenye janga hilo.
Muda mwingine alionekana akisali na kuwashukuru wa okoaji kwani aliamini ataokolewa apo mpaka siku ya tatu ndipo alipo badilika na kuanza kulia mara nyingi kwasabu alikua amesha kata tamaa, damu zili mtoka ndani ya macho baada ya mishipa kupasuka, na macho nayo yalibadilika na kuwa Meusi.
Waokoaji kutokana na hali duni na ukosefu wa vifaa vya uokoaji, walishindwa kwani ilipofika tarehe 16/11/1985, saa 4 na sekunde 5 asubuhi Omayra alikata roho na ndipo Frank Fourmer alipo bahatika kupiga picha hiyo maarufu ya Omayra punde tu kabla ya umauti.
Katika janga hilo zaidi ya watu 23,000 walipoteza maisha.