HABARILEO
Baraza la Mtihani la Taifa NECTA limetangaza matokeo ya darasa la Saba yanaonyesha kuwa ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 6.38 huku Mikoa ya kanda ya Ziwa ikitoa shule nane kati ya kumi bora kitaifa huku shule nyingine mbili zinazokamilisha ufaulu huo zinatoka Dar es Salaam na Kilimanjaro.
Katibu Mtendaji wa NECTA Charles Msonde alisema zaidi ya wanafunzi laki nne kati ya laki nane waliofanya mtihani wamepata alama za juu za 100 na zaidi kati ya alama250 ambayo ni sawa na asilimia56.99 ambapo mwaka jana ufaulu ulikua kwa asilimia50.61.
Hata hivyo alisema wanafunzi zaidi ya laki tatu wamefeli mtihani huo kwa kupata alamaD na E huku wasichana wakifanya vizuri kuliko wanaume.
Aidha alisema takwimu za matokeo zinaonyesha ufaulu katika masomo yote umepanda kwa asilimia kati ya 0.64 hadi 8.94 ikilinganishwa na mwaka jana huku watahaniwa wakifaulu zaidi somo la kiswahili.
HABARILEO
Bunge limeelezwa kuwa deni la walimu linalodaiwa Serikali limeshuka hadi kufikia bilioni4 tu kutokana na mfumo mzuri unaolipwa na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI
Akijibu swali bungeni,la Mbunge wa viti maalumDiana Chololo kuhusu madai ya walimu,Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alisema kwa sasa kiwango hicho kimeshuka hadi kufikia bilioni4 kutoka zaidi ya bilioni60 ambazo zilikua zikidaiwa.
Alisema hatua hiyo inadhihirisha nia njema ya Serikali ya kulipa madeni yote ya walimu kwa lengo la kuboresha maisha yao na hasa baada ya kuboreshwa kwa mfumo wa ulipwaji ambao kwa sasa hautawezesha tena deni hilo kukua.
Alisema lengo la serikali la kulipa moja kwa moja katika akaunti ni kuepuka mishahara hewa inayolipwa kwa watumishi wasiostahili.
MWANANCHI
Wizara ya Maliasili imesema tatizo la ujangili limelisababishia Taifa hasara kubwa kiuchumi inaofikia kiasi cha bilioni1.8.
Naibu waziri wa maliasili Mahamud Mgimwa alieleza hasara hiyo ilikua katika kipindi cha mwaka 2013/14 ambacho wanyamapori205 wa aina mbalimbali waliuawa.
Jambo jingine alisema kuwa ni matumizi makubwa ya rasilimali watu,fedha na muda katika kupambana na ujangil kwenye mbuga mbalimbali za wanyamapori.
Kuhusu doria alisema katika kipindi hicho ilifanyika ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa ikiwemo kuwakamata majangili998 waliofikishwa katika vyombo vya sheria huku wengine wakilipa zaidi ya milioni256 kama fidia.
MWANANCHI
Watu wasiofahamika wamemuua kwa kumkatakata mapanga na kisha kumnyofoa sehemu za siri mwanamke mmoja Hollo Machibula mwenye umri wa miaka54 Wilani Geita.
Diwani wa kata ya Bikandwe Henry Alphonce alisema mwanamke huyo alivamiwa na watu hao majira ya saa5 usiku wakati amelala na kuanza kumkatakata mapanga.
Alisema mwanamke huyo alikua akiishi na binti yake mwenye umri wa miaka25 ambapo wauaji hao walimlazimisha kuingia chini ya uvungu wa kitanda kabla ya kuanza kumshambulia mama yake.
Akisimulia tukio hilo binti huyo alisema alishuhudia mama yake akichinjwa na watu hao kisha kunyofolewa sehemu zake za siri walizotoweka nazo wauaji hao.
Chanzo kinadai mauaji hayo huenda yamesababishwa na ugomvi kati ya marehemu na mumewe ambao wlaikua na ugomvi mkubwa wa kifamilia.
NIPASHE
Mke wa Waziri mkuu Tunu Pinda amesema bado hajashirikishwa na mume wake Mizengo Pinda kuhusu nia ya kiongozi huyo wa nchi kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao mwakani.
Alisema mume wake bado hajatangaza nia hiyo ya kuwania nafasi hiyo kubwa kwani hajawah kukaa na familia yake na kuweka bayana juu ya nia yake ya kutaka urais.
“Mume wangu bado hajatangaza rasmi kuwania uraisi,mimi kama mke wake hajaniambia na hata watoto wake hajawashirikisha,na sisi kama Watanzania tunatakiwa kufahamu uraisi ni baraka toka kwa Mungu hivyo kama atafanya hivyo itakua ni jambo jema”alisema Tunu.
Alisema na hata kama atatangaza kuwania nafasi hiyo na hatimaye kukosa hatajisikia vibaya kwani anaamini nafasi hiyo Mungu ndiye anayepanga nani ataongoza nchi hii baada ya utawala wa rais Kikwete.
JAMBOLEO
Ukata wa fedha ambao umevikumba vikao vya kamati za bunge umesababisha Naibu Spika Job Ndugai kuiomba Wizara ya Fedha kushughulikia posho za wabunge ili walipwe kwa ajili ya vikao vinavyoendelea.
Ndugai alitoa kauli hiyo Bungeni wakati naibu Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba akijibu maswali ya wabunge hao kuhusu Wizara hiyo kwamba ina majibu mazuri na uhakika.
Baadhi ya wabunge hao walionekana kuwa na wasiwasi kuhusu ni lini watalipwa fedha zao huku wakisema hawaielewi Wizara ya fedha ina mpango gani nao mpaka sasa.
MTANZANIA
Shirika la bima la Taifa NIC limekana kudaiwa deni la milioni8.7 na hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambalo limesababisha kukatwa kwa huduma ya matibabu kwa mkopo dhidi ya wafanyakazi wake.
Meneja wa Pensheni na Bima wa shirika hilo Henry Mwalwisi alisema NIC haijapokea taarifa yoyote kutoka Muhimbili kuhusu deni hilo na kwamba taarifa hizo alizisoma kutoka kwenye vyombo vya habari.
Alisema baada ya Taarifa hizo NIC ililazimika kumtuma daktari kwenda kuhakikisha katika ubao wa matangazo wa hospitali hiyo na kukuta ni kweli wanadaiwa deni hilo.
“Alikuja na kutuletea deni hilo la milioni8.7 lakini ninachofahamu mimi tulikua tumelipa na kubakiza milioni2.5 katika deni hilo na ofisi ya muhasibu imeidhinisha deni hilo na kwamba litaingizwa kwenye akaunti ya Muhimbili siku yoyote kuanzia sasa,tunashangazwa na kiasi hicho kikubwa walichotaja”alisema.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook