Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Merdic amefariki katika hospitali ya Mango Jijini Uganda baada ya kuugua ugonjwa Marburg.
Wizara ya Afya nchini humo imesema inashikilia watu79 waliokua karibu na marehemu kutokana na kuhisiwa kuwa na virusi vya ugonjwa huo huku ndugu yake wa karibu aliyekua akimuuguza akihisiwa kuambukizwa ugonjwa huo.
Wizara hiyo ilisema miongoni mwa dalili za ugonjwa huo ni pamoja na homa kali,kuumwa kichwa pamoja na kuharisha mfululizo.
xxxx
Raia wa Uganda Henry Chimuli amefariki dunia katika uwanja wa ndege wa Entebbe baada ya kuanguka kutoka gorofa ya pili katika eneo la kuondokea.
Msemaji wa Polisi Fredrick Enang’a alisema mtu huyo aliangukia mgongo na kuumia kichwa na alifariki muda baada ya kufikishwa katika hospitali ya Grade B ikiwa ni mita chache kutoka uwanjani hapo.
Alisema uchunguzi wa Polisi kuhusu kifo chake unaendelea baada ya kuwepo na utata.
xxxxxx
Ripoti ya mahakama ya Buganda Road imewatupa jela watuhumiwa wa kesi ya vitendo vya ugaidi vilivyofanyika mwezi Septemba nchini Uganda.
Hakimu daraja la kwanza wa mahakama hiyo Saimon Kintu aliamuru watuhumiwa hao kupelekwe ndani katika gereza kuu la Luzira hadi Oktoba23 kesi yao itakapotajwa tena.
Alisema watuhumiwa hao tisa waliokua wamehifadhi eneo la Kireka wakati uchunguzi ukiendelea kati yao watatu ni raia wa Somalia ambapo wawili kati yao ni wanawake na mmoja ni mwanaume aliyekutwa na uraia wa Kenya.
Kintu alisema watuhumiwa hao walikutwa na vifaa vya kutengeneza mabomu katika chimbo moja ambalo walikua wamejihifadhi kwa muda.