MTANZANIA
Mwalimu wa Shule ya Ufundi ya Santa Cacilia ya Mkoani Kilimanjaro Eliuteria Kiwia ameuawa na watu wasiojulikana kisha kumnyofoa macho yake.
Inadaiwa mwalimu huyo alipigwa na kitu kizito kichwani kilichosababisha kifo chake na mwili wake kutupwa katika mfereji wa maji uliopo pembeni ya barabara.
Kamanda wa Polisi Kilimanjaro Koka Moita alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema tukio hilo lilitokea saa sita usiku na mwili wa marehemu kutupwa katika mtaro na ulipokaguliwa ulikutwa na shilingi laki3 pamoja an simu ndogo aina ya Sumsung.
Alisema hadi sasa haijafahamika mali yoyote iliyoibwa na uchunguzi zaidi unafanywa ili kubaini waliohusika na mauaji hayo.
MTANZANIA
Mifuko ya hifadhi ya jamii nchini huenda ikashindwa kuwalipa mafao ya wanachama wake endapo Serikali itaendelea kulimbikiza deni la zaidi ya trilioni8.43 inazodaiwa.
Mkurugenzi Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya jamii (SSRA) Irene Kisaka alisema fedha hizo ni muhimu zikalipwa ili mifuko hiyo iweze kuendelea kufanya uwekezaji.
Alisema ifike wakati Serikali ione umuhimu wa kulipa deni ilo ili liweze kutumika katika shuguli nyingine kwani ni la muda mrefu na linapoteza matumaini ya watumishi.
Alisema mwaka 1996 Serikali ilikopa trilioni7.6 kutoka PSPF ambazo hadi sasa fedha hizo hazijarudishwa.
MWANANCHI
Madereva wa Shirika la Usafiri Dar UDA jana waligoma kushinikiza kupunguzwa kiwango cha fedha cha laki mbili na elfu tano wanachotakiwa kurejesha kwa siku.
Mgomo huo uliokuwapo kwa saa kadhaa kabla ya kutatuliwa na uongozi,madereva hao walikua na madai mawili ikiwemo kugoma kurejesha laki mbili na elfu tano pamoja na kutaka kuongezewa mishahara yao.
Mkuu wa kitengo cha uhusiano cha Shirika hilo George Maziku alisema wanafanyia kazi malalamiko ya watumishi wao na kaunzia January mwakani wataanza kulipa mishahara mipya.
MWANANCHI
Mtu anayedaiwa kuwa kiongozi mkuu wa kundi la watu wanaohusika na matukio ya milipuko ya mabomu na umwagiaji tindikali viongozi wa dini ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati akijaribu kutoroka.
Kamanda wa Polisi Arusha Liberatus Sabas alisema mtuhumiwa huyo Yahya Hassan aliuawa saa5 usiku wakati akiwapeleka askari nyumbani kwake alikoficha mabomu ambapo alijaribu kuwatoroka akitumia uzoefu wake lakini alipigwa risasi na kufia katika Hospitali ya Maunt Meru wakati akitibiwa.
Sabas alisema marehemu alikiri kuhusika na tukio la bomu lililotokea katika kanisa la Mtakatifu Joseph Arusha ambapo watu watatu walifariki huku wengine zaidi ya 60 wakijeruhiwa vibaya.
HABARILEO
Jeshi la Polisi Tanga linamshikilia mtoto mwenye miaka16 kwa kosa la kunywa sumu kwa lengo la kujiua baada ya kunusurika kubakwa na baba yake mzazi.
Kamanda wa Polisi Tanga Frasser Kashai alisema tukio hilo lilitokea Okktoba18 wakati baba yake Richard Leornad alipomvamia kwa lengo la kutekeleza ubakaji huo lakini mtoto huyo alifanikiwa kumtoroka na kuokolewa na wasamaria wema.
Alisema kwa sasa mtoto huyo anatibiwa katika hospitali ya Bombo chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi huku baba yake huyo akishikiliwa na Polisi kwa uchunguzi zaidi.
UHURU
Walimu watano wamefukuzwa kazi na kufutiwa utumishi kati ya hao watatu ni kutokana na makosa ya kujihusisha kimapenzi na wanafunzi wao.
Katibu Msaidizi wa idara ya Utumishi wa walimu Christine hape alisema walimu hao walifukuzwa kazi kutokana na makosa yao kuwa makubwa hivyo kujadiliwa na kutolewa uamuzi huo.
Alisema walimu wengine wamekua na tabia ya utoro uliopitiliza bila kutoa taarifa huku akiwaasa walimu kuacha tabia ambazo zinajenga picha hasi mbele ya jamii pamoja na kufuata kanuni na sheria za kazi kama zilivyowekwa.
NIPASHE
Watu tisa wamewekwa chini ya Karantini kutokana na kumuhudumia mtu anayedaiwa kufariki na ugonjwa wa Ebola Wilayani Sengerema mwishoni mwa wiki iliyopita.
Idadi hiyo imefikia tisa baada ya wafanyakazi watatu Wilayani humo waliohusika kuuzika mwili wa mgonjwa huyo kuzuiwa kuchanganyika na wanajamii hadi vipimo halisi vitakapothibitisha ni ugonjwa gani umemuua msichana huyo.
Mmoja wa wauguzi wa Hospitali Wilayani humo alisema idadi ya waliuowekwa chini ya Karantini imefikia tisa baada ya wanandugu pamoja na wafanyakazi waliomzika kuhisiwa huenda nao wakawa wameambukizwa ugonjwa huo.
Hata hivyo mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo amewatoa hofu wananchi kuhusu kuwepo kwa ugonjwa huo na kusema wanasubiri sampuli za vipimo vya awali toka hospitali ya Muhimbili.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook