MTANZANIA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe limewafukuza kazi askari polisi watatu kwa kosa la kupigana hadharani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Fulgence Ngonyani alisema kuwa askari hao walitimuliwa kazi baada ya kupatikana na hatia kwa kukiuka taratibu za kazi zao.
Alisema askari hao walipigana hadharani saa10 alasiri na jeshi kuamua kutoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watumishi wenye tabia ya kupigana hadharani.
MTANZANIA
Jeshi la Polisi Mkoani Kagera limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama waliojitokeza kumpokea Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la wanawake wa Chadema (BAWACHA) Halima Mdee.
Walilazimika kutumia mabomu ya machozi wakati Mdee alipokwenda kusaini kitabu cha wageni kwenye ofisi za Chama hicho.
Mbali na kutumia mabomu ya machozi pia Jeshi hilo limezuia mikutano yote ya hadhara iliyokua ihutubiwe na Mdee jana kwa madai kuwa hakutakua na usalama wa kutosha.
MWANANCHI
Uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili umesema umepandisha gharama za huduma ya kitanda na chakula ili kuongeza mapato yakatayosaidia kulipa deni la bohari kuu ya dawa MSD
Kauli hiyo ya meneja uhusiano Muhimbili Aminiel Algaesh imekuja siku moja baada ya hospitali hiyo kupandisha gharama na kusema gharama hizo zitasaidia kupunguza deni la bilioni8 wanazodaiwa na MSD.
Alisema baada ya kupitia utaratibi huo ambao ulianzishwa mwaka2003 uongozi uliadhimiai kupanda kwa gharama za utoaji huduma za chakula na malazi hivyo kulazimika kubadilisha mfumo na kumtaka mgonjwa anayelazwa kuchangia5000 kwa siku na chakula2000.
MWANANCHI
Hatimaye mwili wa Rosemary Marandu uliohifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti hospitali ya KCMC Moshi kwa siku53 umezikwa huku maziko yake yakigubikwa na utata na kuhudhuriwa na wanaume sita.
Mazishi hayo yalifanyika juzi katika makaburi na Karanga na hakuna aliyehudhuria kati ya baba na mama wa marehemu huku walomzika kutumia muda mfupi sana kumaliza zoezi la kumzika.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema waliona magari mawili moja likiwa na mwili wa marehemu yakiingia makaburini hapo lakini utata umezidi hukusu ni nani aliyefanya maziko hayo baada ya ndugu wote kususia.
UHURU
Kila Mtanzania nchini atakua na uwezo wa kupata simu za kisasa na yenye uwezo mkubwa (Smartphone) kwa bei ya chini kabisa katika miaka mitano ijayo kuanzia mwaka2020.
Hiyo ni moja ya mipango ya kampuni mpya ya simu inayojiandaa kuingia katika soko la simu Tanzania.
Kampuni hiyo pia imemwambia Rais Kikwete kuwa itasambaza mawasiliano ya Internet kwa kila kijiji nchini na kwamba kwa taasisi za umma kama vile shule,hospitali na vituo vya polisi zitapatiwa huduma hiyo bila malipo yoyote.
Mwenyekiti wa kampuni hiyo ya Viettel toka Vietnam Nguyen Munh amemwambia Rias Kikwete kuwa kampuni hiyo inakusudia kumwezesha kla Mtanzania kumiliki simu hizo kwa punguzo kubwa na pia kupunguza huduma za Internet.
UHURU
Muunganiko wa vyama vinne vya upinzania umeendelea kupokelewa kwa hisia tofauti huku wengine wakiuponda ambapo Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe amesema muungano huo hauna tija kwa Taifa.
Zitto alisema Muunganiko huo ni kwa ajili ya wasaka utawala badala ya uongozi ambao pia wanaweza kuitwa wasaka tonge kwa kutaka kujinufaisha binafsi.
Zitto alisema katika maeneo mbalimbali nchini ,mazao ya wakulima kama mahindi na mpunga yamekua yakiharibika kutokana na kukosekana kwa masoko hivyo kuendelea kuwa maskini.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook