Hospitali ya Taifa Muhimbili imepandisha huduma zake hospitalini hapo na sasa mgonjwa atakayelazwa atalazimika kulipia shilingi 5000 kwa siku.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Marina Njelekela alisema Gharama hizo zitalipwa kwa wagonjwa wote wa rufaaa zilianza tangu Oktoba17 lakini hakufafanua uamuzi wa kupandisha gharama hizo.
Naibu Waziri wa Afya Steven Kebwe alisema hafahamu lolote juu ya ongezeko la bei hizo na anachojua gharama bado zipo chini.
Muuguzi wa Hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake lifahamike alisema gharama hizo zinahusisha malazi 5000 kwa siku na chakula 2000 kwa mlo mmoja,gharama ambazo hazikuwepo siku za awali.
Muuguzi huyo alisema idadi ya wagonjwa wodini kwa sasa imepungua kutokana na wengi wao kushindwa kumudu gharama na kulazimika kujitibu majumbani.
MWANANCHI
Suala la uhaba wa dawa na vifaa tiba katika Hospitali mbalimbali nchini ikiwemo Taasis ya saratani Ocean Road limeonekana kuilemea Wizara ya afya baada ya Wazir Seif Rashid kuthibitisha huku akidai kuwa Serikali itapeleka fedha kwa awamu mbili bohari kuu ya dawa ili kudhibiti uhaba huo.
Waziri Seif alikiri kuwa kweli MSD inaidai Serikali kiasi cha bilioni90 jambo ambalo linaifanya bohari hiyo kushindwa kununua dawa kutoka kwa wauzaji ndani na nje ya nchi na Serikali imekua ikitoa kiasi kidogo kidogo ili kuongeza uwezo wa bohari hiyo kununua na kusambaza dawa.
Waziri huyo alikiri kuwepo na ukosefu wa matibabu kutokana na ukosefu wa dawa pamoja na ubovu wa baadhi ya mashine za mionzi.
Rashidi alizitaka hospitali kuhakikisha kuwa zinapeleka asilimia 50 ya mapato licha ya kuwa Wizara inapeleka fedha MSD kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba.
MWANANCHI
Utafiti mpya unasema kusengenya ni tiba katika mwili kwa sababu unatoa fursa kwa nafsi kujilinganisha na watu wengine hasa wanaowaonea donge hivyo hupunguza mawazo na magonjwa yanayoweza kusababishwa na mambo yanayokufanya ukose Amani.
Mtafiti wa chuo kikuu Groningen Profesa Elena Martinescu alisema usengenyaji unamsaidia mtu kujilinganisha na kujitazama na watu wanaomzungumzia katika vikao vyake vya kueneza majungu.
Utafiti huo unasema pia maneno ya umbeya ambayo huwa mabaya humuandaa mtu anayepewa taarifa hizo akiamini kuwa hata yeye kama akifanya hivyo anaweza kuwa mlengwa wa majungu.
Utafiti huo pia umeeleza kuwa wanaume wengi hivi sasa hawawezi kutunza siri tofauti na ilivyokua awali kuwa ukimwambia mwanamke habari itasambaa baada ya muda mfupi na sasa kibao kimewageukia wanaume na ukitaka habari isambae haraka basi mwambie mwanaume.
JAMBOLEO
Rais Jakaya Kikwete amesababisha mageuzi makubwa kwa namna Serikali ya watu wa China inavyowapokea viongozi wageni kutoka nje ya nchi hiyo kwa kuwa kiongozi wa kwanza duniani kupokelewa kwa pikipiki za polisi na kuongozwa kwa muda wote wa ziara yake katika kipindi cha miaka10 iliyopita.
Kikwete ambaye aliwasili nchini China Oktoba21 na kuanza ziara ya siku sita nchini humo amekua kiongozi wa kwanza wa nje kupokelewa kwa msafara wa pikipiki tangu 2004 wakati China ilipofuta utaratibu wa misafara ya viongozi kusindikizwa kwa pikipiki za polisi.
Taarifa ya habari iliyotolewa na Wizara ya mambo ya nje ya China haikutoa sababu zozote za mabadiliko ya sera hiyo.
Karibu nchi zote duniani utaratibu wa viongozi wa nchi mbalimbali hupokelewa kwa misafara ya pikipiki ni protokali ya juu kabisa ambayo pia huongeza usalama wa kiongozi na ni utaratibu wa kawaida katika nchi nyingi duniani.
MTANZANIA
Watahiniwa binafsi wa mitihani ya kidato cha nne sasa watalazimika kufanya mitihani miwili kwa kila somo ambapo mmoja utakua na alama70 nawingine30.
Meneja utawala wa Baraza la Mitihani la Taifa Daniel Mafie alisema watahiniwa binafsi wamekua wakifanya mtihani mmoja ambao unachukua alama zote 100 tofauti na watahiniwa kutoka shuleni ambao wao mtihani wa mwisho una alama70 na tathmini za maendeleo zina alama30.
Alisema mfumo wa awali ulikua unawaumiza watahiniwa wa kujitegemea ambapo kama mtihani wa mwisho ukiwa mgumu sana wengi wanafeli huku wengine wakipata alama za tathmini za maendeleo.
Kwa upande mwingine NECTA imeweka utaratibu wa utoaji vyeti mbadala kwa waliopoteza vyeti vyao vya taaluma.
MTANZANIA
Mwili wa marehemu unaokadiriwa kuwa na miaka30 umekutwa ukiliwa na mbwa katika kijiji cha Lupapira Mkoani Ruvuma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema mbwa hao walikutwa na mkazi wa kijiji hicho aliyekua akienda porini kwa shughuli zake binafsi.
Alisema tukio hilo lilitokea saa 9 alasiri nje kiogo ya Manispaa ya Songea ambapo baada ya mkazi huyo kuona viungo vya binadamu vikiliwa na mbwa hao ndipo alipotoa taarifa kwa uongozi wa Serikali ya Mtaa ambapo waliwasiliana na Polisi waliofika eneo hilo wakiwa wameongozana na daktari.
Daktari huyo alipovifanyia uchunguzi viungo hivyo alibaini marehemu alipigwa na kitu kizito kichwani kilichopelekea kifo chake.
HABARILEO
Mbunge wa Ubungo John Mnyika amemtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye ni msimamizi mkuu wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Disemba mwaka huu kufanya marekebisho ya kanuni za uchaguzi huo kinyume na hapo atafungua kesi mahakamani kupinga kanuni hizo.
Mnyika alitoa mfano wa mapungufu ya kanuni hizo ni ukomo wa muda wa kufanya mikutano ya hadhara wakati wa kampeni kuwa mwisho saa11 jioni badala ya saa12 kama ilivyokua kawaida ya mikutano yote.
Alisema kanuni hizo za uchaguzi zinamtaka mpigakura kuandika kwa kujaza majina ya wagombea wakati wa kupiga kura jambo ambalo alisema linaweza kusababisha usumbufu mkubwa kwani ni vigumu kwa mwananchi kushika kichwani majina saba ya wagombea na kuyajaza yote.
MTANZANIA
Kocha mkuu wa Siba Mzambia Patrick Phiri amesema yupo tayari kujiuzulu kuendeela kuifundisha timu hiyo endapo itashindwa kuibuka na ushindi katika mechi tatu zijazo za ligi kuu Tanzania bara.
Mechi hizo ni dhidi ya Mtibwa Sugar,Ruvu Shooting na Kagera sugar kama uongozi wa Simba ulivyotaka.
Uongozi wa Simba ulimpa majukumu ya kuhakikisha Simba inafanya vizuri katika mechi tano za awali lakini mambo yamekua ni tofauti kutokana na matokeo ya sare mfululizo.
Phiri alieleza masikitiko yake ya kupata matokeo yasiyoridhisha huku akiwatupia lawama wachezaji wake kwa kutokua makini uwanjani.
MWANANCHI
Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali PC jana iligeuka mwiba kwa watendaji wa Shirika la maendeleo ya Petrol nchini TPDC,Kampuni ya Ranchi ya Taifa NARCO na Wizara ya Nishati na Madini baada ya kuwatimua wakurugenzi na wenyeviti wa bodi kwa kushindwa kutoa maelezo ya kutosha kuhusu ubadhirifu wa fedha za uma,uzembe na wizi.
Katika uamuzi wake,Kamati hiyo iliyopo chini ya Zitto Kabwe iliwatimua watendaji wa TPDC baada ya kushindwa kuwasilisha mikataba26 ya gesi na mapitio yake kama walivyoagizwa na kamati.
Zitto alianza kwa kumtaka Mwenyekiti wa bodi ya TBDC kueleza sababu za kutowasilisha mikataba hiyo na kujibiwa kwamba mikataba ya Serikali ina utaratibu wake wa kuipata.
Kauli hiyo ilichafua hali ya hewa na kumlazimu Zitto na makamu wake kueleza kuwa sheria ya Kinga,haki na madaraka ya bunge inaruhusu kamati kupata taarifa yoyote ile.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook