Wakati bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania likiendelea na vikao vyake mjini Dodoma,imeelezwa kwamba nusu ya wabunge239 wa kuchaguliwa waliopo sasa watabwagwa katika uchaguzi mkuu ujao 2015.
Hiyo inatokana na wabunge wengi kutoa ahadi nyingi kwa wapigakura ambazo hazitekelezeki hivyo kukumbwa na rungu la wananchi mwakani.
Hayo ni matokeo ya utafiti wa Twaweza yaliyotolewa jana Jijini Dar es salaam ambayo yanaonyesha Watanzania nane kati ya10 hawawafahamu kwa majina wala vyama Wabunge wao.
Mtafiti Elvis Mushi alisema nusu ya Watanzania walipoulizwa kama watawapigia tena wabunge wao kura katika uchaguzi mkuu mwakani walisema hapana kwani hawajaona walichofanya kwa kipindi walichokaa madarakani.
MWANANCHI
Muungano wa vyama vya siasa vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi Ukawa huenda ukapata nafasi kubwa katika uchaguzi mkuu mwakani,Utafiti wa Twaweza umebainisha.
Utafiti huo umebainisha kuungana kwa vyama hivyo ambavyo ni CUF,CHADEMA,NCCR-Mageuzi na NLD utaongeza ushindani wa kukitisha Chama tawala cha CCM ambacho kina ngome imara.
Nusu ya Watanzania waliohojiwa waliotaka kubainisha iwapo wapinzani wangesimamisha mgombea mmoja wangemchagua nani,walisema wangechagua CCM na karibu theluthi wangemchagua mgombea wa upinzani.
Pamoja na mapendekezo hayo bado karibu kila watu wawili kati ya 10 walioulizwa nani anafaa kuwa rais kupitia upinzani jambo ambalo linaweza kubadilisha matokeo hayo ya urais katika dakika za mwisho.
MWANANCHI
Mfanyabiashara maarufu nchini Mohammed Dewji ametajwa kuwa ndiyo bilionea namba moja nchini kwa sasa akifuatiwa na Rostam Aziz.
Kwa mujibu la jarida la Ventures la Afrika lililotolewa jana,wafanyabiashara hao ndio Watanzania pekee walioingia kwenye orodha hiyo ya mabilionea55 barani Afrika.
Dewji ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mjini kwa tiketi ya CCM ni mfanyabiashara kijana aliyekamata nafasi ya 24 katika orodha hiyo akiwa na utajiri wa dola za Marekani bilioni2 sawa na trilioni3.
Nafasi hiyo inamfanya kijana huyo kutambulika kama tajiri namba moja nchini kwa sasa na si Rostam tena.
MTANZANIA
Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS imetoa ripoti inayoonyesha kuwa kundi la vijana wenye umri wa miaka15-19 lipo katika hatari Zaidi ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo.
Hata hivyo inaonekana kuwa tofauti kwa kundi la wazee ambapo maambukizi yamepungua kutoka asilimia 7 mwaka2012 mpaka asilimia54 mwaka 2014.
Ripoti hii inaeleza kuwa kitaifa vifo vitokanavyo na ugonjwa huo vimepungua kwa asilimia50 ikiwa ni kutoka vifo 140,000 mwaka2005 hadi80,000 mwaka 2013.
Ripoti hiyo inasema sehemu kubwa ya Watanzania bado hawajui hali zao za kiafya na wala hawajawahi kupima,jambo linalotia shaka kuhusu ukubwa wa tatizo hilo katika jamii.
MTANZANIA
Hivi karibuni taasis ya Envirocare ya Dar es salaam imefanya utafiti katika Mikoa saba kuhusu matumizi ya bidhaa za vipodozi kwa afya ya binadamu na mazingira uliobainisha kwamba asilimia52 ya Watanzania hutumia vipodozi vyenye sumu.
Mikoa hiyo ni pamoja na Arusha,Mwanza,Dodoma,Mbeya,Tanga,Singida na Dar es salaam ambapo mwaka 1964 wenye umri kati ya miaka15 walihojiwa.
Akifafanua matokeo ya utafiti huo mratibu wa kupunguza madhara ya kemikali katika taasis hiyo Euphrasia Shayo anasema kati ya watu hao waliohojiwa watu 567 wamekubali kuwa wanatumia vipodozi ili kufanya ngozi iwe nyororo na laini,419 walisema wanatumia ili ngozi iwe nyororo,367 wanatumia ili kukuza nywele na ziwe stahivu.
Shayo alisema utafiti huo pia umeonyesha wateja wakubwa wa bidhaa hizo ni wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini pamoja na wasanii tofauti hasa wa muziki pamoja na waigizaji.
HABARILEO
Mizani ya madeni ya Shirika la ndege Tanzania ATCL imepungua kutoka shilingi bilioni133 hadi bilioni40 hivi sasa hatua inayotoa matumaini kwa shirika hilo kuingia kwenye ushindani karibuni.
Katika hatua nyingine kuboreshwa kwa mazingira ya biashara ya anga nchini kumefanya mashirika ya ndege duniani kuomba ndege zao kutua mara tatu nchini kutoka mara moja kwa siku kama ilivyokua nyuma.
Naibu Waziri wa uchukuzi Charles Tizeba alisema juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kufanya sekta hiyo kuwa bora kwa kuboresha mazingira yenyewe lakini pia kuiboresha ATCL.
Alisema deni kubwa lililokua linaikabili ATCL lilikua kikwazo kikubwa katika kulifanya kufufuka na kutoa ushindani ,lakini kazi kubwa ilikua imefanywa katika kurekebisha mizani ya madeni.
HABARILEO
Serikali imesema Tanzania haina sheria ya kuwaruhusu wafungwa kukutana faragha na wenza wao.
Hii ni mara ya tatu kwa Serikali kutoa majibu hayo kutokana na maswali ya ambao mara kadhaa wamekua wakihoji kwanini hakuna sheria hiyo.
Hata hivyo Naibu Waziri wa mambo ya ndani Pereira Ame alikiri kwa Tanzania kutokuwepo na sheria hiyo na kujibu ujauzito ambao huwapata wafungwa wa kike unatokana na kuupata wakiwa nje ya magereza.
Kuhusu tuhuma za kulawitiwa kwa Masheikhe wa Zanzibar alisema suala hilo linafanyiwa uchunguzi na tayari wamefanyiwa vipimo katika hospitali ya Amana.
NIPASHE
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amesema hana ugomvi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kwa kuwa amemlea na kumsaidia vituvingi ikiwemo fedha,gari,kula na kulala nyumbani kwake.
Mbowe alisema Chama hicho hakijamtenga Zitto bali yeye mwenyewe ndiyo alijitenga na kufafanua kuwa Chadema hakiwezi kujengwa na viongozi ambao ni wapenzi wa Chama cha Mapinduzi.
“Kuna baadhi ya watu wanajua mimi nampiga vita Zitto kwa kuwa nimemlea,amekula na kulala nyumbani kwangu na mimi ndiye niliyemshauri kugombea Ubunge na kumpa fedha na gari kwa ajili ya kufanya kampeni,,iweje leo nimpige vita?alihoji Mbowe.
NIPASHE
Waziri mkuu wa Zamani Edward Lowassa amewaburuza makada wenzake ndani ya Chama cha Mapinduzi kwa wanan chi wengine kuonyesha kwamba wangemchagua kuwa Rais kama uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge unge fanyika sasa.
Utafiti huo uliofanywa na Taasis ya Twaweza yaliyotolewa na mtafiti Elvis Mushi alisema wananchi 1445 waliohojikwa kwa njia ya simu asilimia13 walisema wangemchagua Lowassa huku asilimia12 wakisema wangemchagua Waziri mkuu Mizengo Pinda.
Utafiti huo ni wa tatu kufanywa na Taasis ya Twaweza na mwaka 2012 Lowassa alikua anakubalika kwa asilimia sita na mwaka jana asilimia13 sawa na mwaka huu.
Watu wanne kati ya 10 ambao ni sawa na asilimi41 walipoulizwa walisema Dk Slaa anafaa kupeperusha bendera ya Ukawa na wengine waliopata asilimia Zaidi ya10 ni Profesa Ibrahimu Lipumba asilimia14 Mbowe asilimia11 na asilimia6 Zitto.
UHURU
Waziri wa Uchukuzi Harrison Mwakyembe amempasha Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu kuwa hana ubavu wa kumng’oa katika nafasi yake ya Ubunge.
Mkwakyembe ambaye ni Mbunge wa Kyela alisema madai ya sugu kuwa atafanya kampeni ya kumwondoa katika jimbo lake katika uchaguzi mkuu ujao ni sawa na mende kuangusha kabati.
Pia amesema uzee kamwe haumuondolei sifa ya kuwa kiongozi na kwamba wenye mawazo hayo wanapaswa kuachana nayo.
Mwakyembe alisema Sugu anadai alikwenda Kyela kwa ajili ya kufanya kampeni kwa za kumng’oa na kusisitiza hata angefanya mikutano mingapi bado ataendelea kutawala katika jimbo lake kwa kuwa wananchi wake wanajua nini anafanya.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook