Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye ametangaza kuvifungia vituo viwili vya radio kwa muda usiojulikana ambavyo ni Magic Fm ya Dar es salaam na Radio 5 ya Arusha kwa makosa ya kutangaza na kutoa habari za kichochezi.
Lakini pia Waziri Nape amesema huku adhabu hiyo ikianza leo August 29 2016 pia ameiagiza kamati yake kuviita vyombo hivyo kwa ajili ya kuzungumza navyo kisha maamuzi mengine ya kisheria yatachukuliwa.
'Nimevifungia vituo viwili vya radio ambavyo ni Radio 5 Arusha na Magic Fm Dar kwa muda usiojulikana kwa kosa la uchochezi' –#Waziri Nape
— millardayo (@millardayo) August 29, 2016
'Nimeelekeza kamati ya maudhui kuviita vyombo hivyo na kuwasikiliza kwa kina kisha kunishauri hatua zaidi ya kuchukua' –#Waziri Nape
— millardayo (@millardayo) August 29, 2016
'Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo August 29 2016 hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake' –#Waziri Nape
— millardayo (@millardayo) August 29, 2016
'Sisi kama Serikali tunatambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari ktk kuleta amani, umoja, mshikamano kwakuwa ni muhimu sana'-#Waziri Nape
— millardayo (@millardayo) August 29, 2016
'Kimsingi radio zote mbili kwa pamoja wametangaza na kutoa habari ambazo zina uchochezi ndani yake'-#Waziri_Nape
— millardayo (@millardayo) August 29, 2016
ULIIKOSA HII TAARIFA YA POLISI DAR KUHUSU MAUAJI YA ASKARI MKURANGA