Imeelezwa kuwa uwepo wa changomoto ya msongo wa mawazo kwa wanaume wengi kwenye jamii imekuwa chanzo cha wanaume kufariki mapema zaidi ya wanawake ikiwa ni miaka saba nyuma ya mwanamke.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Mtandao wa Ushiriki wa Wanaume Tanzania (MEN ENGAGE TANZANIA) Viola Husiri wakati wa kutoa mafunzo ya Afya Akili kwa baadhi ya vijiwe vya Bodaboda Jijini Dar es salaam ambapo amesema ni muhimu kwa jamii kupewa elimu ya mahusiano ya familia ili kujenga usawa kwani endapo ukikosekana unapelekea wanaume kuangukia katika ukatili.
Hata hivyo Mwenyekiti amebainisha kuwa katika mafunzo hayo wanawafundisha boda boda masuala ya afya ya akili kutokana na kundi hilo kukutana na changamoto za misongo ya mawazo katika zao hasa kufuatia kubeba makundi na watu wa aina tofauti tofauti.
Naye mwakilishi wa boda boda Charles Everest kijiwe cha Sinza amesema msongo wa mawazo umekuwa ukipelekia baadhi yao kuchukua maamuzi magumu hivyo baada ya kupata elimu ya afya ya akili itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuishi vizuri na jamii.
STRESS ZINACHANGIA WANAUME KUFARIKI MAPEMA KULIKO WANAWAKE, BODABODA WAPEWA SOMO AFYA YA AKILI