MWANANCHI
Siku ya kesho Desemba 07 kutafanyika Onyesho kubwa la Mavazi la Swahili Fashion Week ambalo limeandaliwa na Kampuni ya 361 Degrees.
Katika maonyesho hayo kutakuwa na utoaji wa tuzo ya ‘Mtu Mwenye Ushawishi Mkubwa katika Mitindo’ ambapo washiriki wa kike waliotajwa kuwania tuzo hiyo ni Mwamvita Makamba, Wema Sepetu na Millen Magesse.
Washiriki wa kiume ni Juma Jux, Diamond Platnumz pamoja na Luca Neghesti, Baraka Shelukindo, Noel Ndale na Rio Paul.
Washiriki katika kipengele cha ‘Mbunifu Bora wa Mchango wa katika Mitindo’ ni Martin Kadinda, PSJ Couture, Mtani Nyamakababi, Manju Mitta na Gabriel Mollel.
Kwa upande wa ‘Mbunifu Bora wa Mavazi wa Mwaka’ wanaowania ni pamoja na Martin Kadinda, Gabriel Mollel, An Nisa Abayas, na Eve Collections.
Kipengele cha ‘Mwanamitindo Bora wa Kike’ ni Jamilla Nyangassa, Gyver Meena, Jihan Dimachk, Neema Kilango, Joceline Maro na Lethina Christopher.
Kwa upande wa ‘Mwanamitindo Bora Afrika Mashariki’ ni Vivian Mutesi, Sharon Mirembe Sanya wote kutoka Uganda, Christina Masese na Ajuma Nasenyana wa kutoka Kenya.
Vipengele vingine ni pamoja na mbunifu bora wa mwaka, tuzo ya mtaalamu wa urembo na nywele, tuzo ya vidani na tuzo ya mbunifu wa Afrika Mashariki.
MWANANCHI
Huenda hata watu wa tabaka la chini wanapendelea maisha mazuri na juu na elimu bora ambapo katika eneo la Buguruni Dar, kumeanzishwa shule ya English Medium ambayo imepewa jina la ‘Perfect Day Care Centre English Medium Nursery School’.
Hezron Mwaisemba ambaye ndiye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo amesema alianzisha baada ya kupata eneo ambalo amefanikiwa kujenga majengo manne ambayo anafundisha wanafunzi wa Chekechea na mpaka sasa tayari jumla ya wanafunzi 125 wamehitimu na kujiunga shule mbalimbali za msingi.
Mwaisemba amesema baadhi ya changamoto ambazo anakutana nazo katika kazi hiyo ni pamoja na kukosa madawati ambapo wanafunzi wanakaa kwenye mikeka pamoja na ukata wa fedha unaosababishwa na baadhi ya wazazi kuchelesha malipo ya ada.
Wazazi wa watoto wanaosoma katika kituo hicho wameonekana kuridhishwa na maendeleo ya kimasomo ya watoto wao, huku masomo yote yakifundishwa kwa lugha ya kiingereza.
NIPASHE
Viongozi wa Mila wa Jamii ya Kabila la Wamasai eneo la Loliondo, Wilaya ya Ngorongoro wamelaani baadhi wa viongozi wa Jamii hiyo ambao wanaunga mkono Serikali na wawekezaji ambao wamechangia katika migogoro ya ardhi ambapo wazee hao wamegoma kusaini mkataba wa kuiruhusu kampuni ya Ortelo Business Corporation kufanya uwindaji Loliondo.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Elias Lali amesema Serikali ilishazungumzia msimamo wake juu ya suala hilo na kusema kuwa ametoa amri ya kupiga marufuku kufanyika mkutano wowote wa hadhara ndani ya eneo hilo mpaka baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa.
NIPASHE
Kada wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kunduchi, Kinondoni Dar amewataka wananchi wasimchague mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mtongani kupitia CHADEMA kwa kudai kuwa aliwahi kuiba sadaka na pia ni mdaiwa sugu wa SACCOS ya Amani.
Kada huyo Livinus Gutambi amesema mgombea huyo Poweli Mfinanga aliwahi kuiba sadaka kanisa la walokole la Doricas na akatimuliwa kusali kanisani hapo.
“ushahidi wa yote haya ninayoongea hapa upo, hivyo niwaombe wananchi wa Mtongani mkataeni mgombea huyo maana si msafi wa kuweza kutuletea maendeleo”—Gutambi.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook