Meneja Sebastian Hoeneß amesema klabu hiyo ‘itamkosa’ na ‘anajuta’ kumpoteza kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 na nahodha wa klabu.
Lakini anakiri kuwa ni ndoto kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Japan kujiunga na Reds na kutimkia Ligi ya Premia na mpango huo una maana kwa klabu zote mbili.
“Wataru Endo ameidhinishwa na klabu kwa ajili ya mazungumzo,” Hoeneß alisema katika taarifa kwenye Twitter.
“Alisafiri kwa ndege hadi Uingereza kwa uchunguzi wa afya na hakuwa mazoezini leo.
“Akiwa na umri wa miaka 30 sasa ana fursa ya kujiunga na Liverpool kwenye Ligi Kuu ya Uingereza. Ni ndoto yake.
“Kwa mtazamo wa klabu, tunazungumza juu ya kifurushi kizuri kiuchumi. Kutoka kwa mtazamo wa michezo, bila shaka, sifurahi. Wataru ni mchezaji muhimu kimchezo na kibinafsi. Yeye ni nahodha wetu.
Amecheza mechi 99 kati ya 102 zinazowezekana za Bundesliga.
“Lakini sitaanza kulalamika. Tunajuta kwa sababu tutamkosa kimichezo. Hata hivyo, tuna uhakika kwamba tutaweza kufidia hili kwa muda mfupi. Tuna uwezekano wa kulitatua ndani kwa nguvu kali. Kwa muda mrefu tunatafuta mbadala wake.”