Mbunge wa jimbo la Geita Joseph Kasheku Musukuma akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ameishauri serikali ione namna kutatua suala la kikokotoo akidai kinawaumiza watumisi wanaositaafu na kusema suala hilo lisiposhughulikiwa litaendelea kutengeneza watumishi wezi.
“Watanzania wanaliamini bunge lakini kuna vitu vinakuwa vinazungumzwa tunaona kama haviwaumizi wananchi lakini kwa uelewa wangu kama daktari wa akili naona tunatengeneza taifa la watumishi wezi maana wanalalamika kila siku suala la kikokotoo mimi sijasoma sana lakini nikiangalia mtu anapata asilimia 30 halafu 70 unamtunzia kama alikuwa analipwa mafao ya asilimia 100 anakuja kutoka na 30 ndio akaanze kujenga ka’SLOP’ lazima niibe tu kwasababu najua hela zangu kule sitapewa” Mbunge Jeseph Msukuma
Tazama pia…