Nchini Sudan, huku mzozo ukigawanya nchi hiyo kwa mwezi wa 4 mfululizo, afisa wa misaada ya kimataifa alihimiza jumuiya ya kimataifa, Jumapili, kutoa fedha zaidi kusaidia watu wa Sudan.
Kulingana na Katibu Mkuu wa Msalaba Mwekundu, ni 7% tu ya rufaa ya dola milioni 45 ndiyo iliyopokelewa.
“Wito kwa washirika wetu na wafadhili ni kwamba mahitaji ni ya kweli, watu wanateseka nchini, hali inazidi kuwa mbaya, na wanahitaji msaada wa haraka.
Zaidi ya watu milioni 3.4 walikimbia makazi yao ndani na zaidi ya milioni moja walivuka kwenda nchi jirani.
Misri ilipokea zaidi ya wakimbizi 250,000 wa Sudan kufikia Agosti 1, kulingana na takwimu rasmi.
“Uendeshaji wa mpaka kwa upande wa Misri umejipanga zaidi kwa sasa ukilinganisha na ilivyokuwa miezi michache iliyopita, pia idadi ya watu wanaokimbia na kuvuka mpaka haiko sawa, niliambiwa ni kati ya 400 na 600 kwa siku sasa, ilipokuwa maelfu mwanzoni.
Hivyo ukilinganisha na siku za mwanzo za (mapigano), katika mazingira yenye changamoto ya kusimamia mtiririko wa watu wengi, hivi sasa inaonekana kujipanga vizuri zaidi.Lakini wakati huo huo , pia niliona na kusikiliza watu ambao wamevuka mpaka, ni kwamba kuna foleni ndefu upande wa pili wa mpaka ili kupita,” aliongeza afisa huyo wa Msalaba Mwekundu.
Sudan ilitumbukia katika machafuko mwezi Aprili wakati mvutano kati ya wanajeshi wa Abdel Fattah Burhan, na wanamgambo wa Mohammed Hamdan Daglo, kulipuka na kusababisha mapigano ya wazi katika Khartoum na miji mingine.