Pande mbili zinazopigana nchini Sudan, jeshi la taifa SAF na wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF), zimekubaliana kusitisha mapigano kwa saa 72 kuanzia Jumapili, diplomasia ya Saudia imetangaza Jumamosi.
Ufalme wa Saudi Arabia na Marekani zimetangaza makubaliano ya wawakilishi wa Vikosi vya Wanajeshi wa Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kwa ajili ya kusitisha mapigano kwa muda wa saa 72 kuanzia Jumapili Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudia imetangaza.
Makubaliano kadhaa ya kusitisha vita hapo nyuma yamekuwa yakivunjika.
Mnamo mwisho wa mwezi Mei, Marekani iliwawekea vikwazo majenerali wanaohasimiana wa pande hizo mbili, ikiwashutumu kwa kile ilichokiita umwagaji damu wa kutisha.
Tangu Aprili, mapigano kati ya jeshi na kikosi cha RSF, yamekuwa yakiendelea mara kwa mara katika mji mkuu Khartoum na jimbo la magharibi Darfur huku pande husika zikikiuka makubaliano ya usitishaji vita yanayolenga pia kutatua tatizo la mgogoro wa kibinadamu uliosababisha mauaji ya zaidi 2000 Makubaliano kadhaa ya kusitisha vita hapo nyuma yamekuwa yakivunjika.
Mnamo mwisho wa mwezi Mei, Marekani iliwawekea vikwazo majenerali wanaohasimiana wa pande hizo mbili, ikiwashutumu kwa kile ilichokiita umwagaji damu wa kutisha.
Tangu Aprili, mapigano kati ya jeshi na kikosi cha RSF, yamekuwa yakiendelea mara kwa mara katika mji mkuu Khartoum na jimbo la magharibi Darfur huku pande husika zikikiuka makubaliano ya usitishaji vita yanayolenga pia kutatua tatizo la mgogoro wa kibinadamu.