Marekani imeiondoa rasmi Sudan kwenye orodha yake ya nchi zinazounga mkono ugaidi, hatua ambayo imechukuliwa jana Jumatatu.
Sudan kuwa wenye orodha hiyo kulizuia nchi za kigeni kufanya biashara na kuwekeza nchini humo kwa kuogopa vikwazo.
Sudan iliwekwa kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi tangu mwaka 1993, ubalozi wa Marekani jijini Khartoum umetangaza kwenye ukurasa wake wa Facebook.
“Wakati kipindi cha siku 45 cha taarifa kwa Bunge kimeisha, KWaziri wa mambo ya Nje wa Marekani ametia saini taarifa ya kuindoa Sudan kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi. Hatua hiyo inaanza kutumika Desemba 14”
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amebaini kwamba kuondolewa rasmi kwa Sudan kwenye orodha nyeusi ya Marekani ni “mabadiliko ya kimsingi” katika uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
“Tunakaribisha ujasiri wa wananchi wa Sudan kwa kutetea uhuru, amani na haki na tunawapongeza wajumbe wa serikali ya mpito inayoongozwa na raia kwa ujasiri wao katika kujibu matakwa ya raia wenzao” Mike Pompeo