Ripoti kutoka nchini Sudan zinasema mapigano yamezuka katika maeneo yote ya mji mkuu muda mfupi kabla ya usitishaji vita wa siku tatu kukamilika mapema asubuhi.
Mapigano makali yamezuka tena wenye mji mkuu wa Sudan, Kahrtoum mapema leo wakati masaa 72 ya makubaliano ya kusitisha mapigano yakifikia mwisho, makubaliano ambayo, hata hivyo, yalikuwa yakivunjwa mara kwa mara.
Walioshuhudia wanasema jeshi la Sudan na kundi pinzani la Rapid Support Forces (RSF) walikabiliana mjini Khartoum.
Makubaliano ya hivi punde yaliafikiwa na Saudi Arabia na Marekani ambapo kumekuwa na ripoti za ukiukaji wa muafaka wa usitishaji wa vita kutoka pande zote mbili.
Pande hasimu nchini ziliaanza kukabiliana mwezi Aprili, mapigano ambayo yameripotiwa kusababisha vifo vya watu kadhaa wengine wakiwa wameyakimbia makazi yao.
Kwa mujibu wa jeshi, wapiganaji wa RSF walitekeleza shambulio kwenye jengo hilo, wakati RSF nayo ikieleza kuwa jengo hilo “lililopo chini ya udhibiti wake” lilikumbwa na mashambulio ya angani na mizinga ya jeshi.
RSF katika taarifa ilishutumu jeshi la Sudan kwa “jaribio la wazi la kufuta ushahidi wa matendo yao ya kikatili wakati wa utawala wao wa kidhalimu”.
Makao makuu ya kijasusi yapo katika jengo moja na wizara ya ulinzi, makao makuu ya jeshi na makazi ya rais.
Jeshi rasmi la Sudan chini ya Jenerali Abdel-Fattah Burhan na Kikosi cha Dharura cha RSF chini ya Mohamed Hamdan Dagalo wamekuwa wakipambana kwa zaidi ya miezi miwili kuwania udhibiti wa madaraka, wakitumia silaha nzito nzito ambazo zimezigeuza baadhi ya sehemu za miji mikubwa nchini humo kuwa magofu.
Mapambano yao yamechochea ghasia kusambaa kwenye jimbo la magharibi la Darfur na kusababisha zaidi ya watu milioni 2.5 kukimbia nchi.