Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) ameweka wazi kuwa atawania tena kinyanganyiro cha Ubunge kwa kuwa bado wanamuhitaji
Amesema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Sido lililopo ndani ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya, ameeleza Kuwa bado ana jukumu zito la kuwatumikia wananchi hivyo mwezi oktoba lazima atagombea tena.
Aidha Mbunge Ametoa msaada wa Shilling 1,000,000 kwa ajili ya kuzibua mifereji ya soko la sido na ujenzi wa ofisi za soko.