August 5 2016 Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu alifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu, Dar es salaam na kusomewa mashitaka matatu likiwemo la kutoa kauli za uchochezi nje ya mahakama hiyo August 2 2016 dhidi ya Serikali iliyopo madarakani.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo Lissu ambaye alikuwa akijitetea mwenyewe kufuatia mawakili wa serikali kupinga uhalali wa wakili Peter Kibatala aliyeteuliwa kumtetea kuwekewa pingamizi lakuwa na yeye ni mmoja wa mashahidi wa tuhuma hizo, Lissu alikubali mashitaka yote kuwa ni ya kweli isipokuwa hakuvunja sheria yoyote.
Baada ya kusikiliza pande zote za mashitaka na mshitakiwa ndipo hakimu mfawidhi Cyprian Mkea akatatoa maamuzi ya kumtaka Lissu kujidhamini mwenyewe kwa malipo ya shilingi milioni 10 ambazo alizilipa na kuachiwa huru huku tarehe ya kusomewa shitaka ikitajwa kuwa ni August 19 2016.
ULIIKOSA HII KAULI YA TUNDU LIZZU BAADA YA KUTOKA MAHAKAMANI