Tunayo stori kutokea kwa Makamu Mkuu wa Taasisi ya Kusimamia Vihatarishi nchini, Buyamba Buyamba ambapo amesema nchi imekuwa ikipata vihatarishi vingi ikiwemo cha Kimbunga Kenneth, huku kwa sasa nchi ikikabiliwa na vihatarishi vya Kiusalama mtandaoni.
Amesema kihatarishi cha mtandaoni kinatokana na mfumo wa malipo yanayofanyika serikali na katika taasisi mbalimbali kwa njia ya Digitali, huku uhalifu wa kimtandao nao ukiongeza.
“Kihatarishi kama cha Kimbunga tulishaenda TMA na tukawafundisha kuhusu vihatarishi hata kabla ya kutangazwa, hivyo kuna timu kubwa pale TMA na tushaielekeza,“amesema