Baada ya headlines za muda mrefu na kuhusishwa kwa nyota wa timu ya taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimovic kuwa atabadili mawazo yake ya kustaafu na kuichezea timu yake ya taifa ya Sweden katika fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, leo April 26 2018 zimetangazwa taarifa tofauti.
Kiongozi wa FA ya Sweden Lars Richt baada ya kufanya mazungumzo ya kina na Zlatan Ibrahimovic ameamua kutoa majibu hadharani kuwa nyota huyo amekataa kubadili mawazo yake ya kustaafu na kurudi timu ya taifa kuichezea fainali za Kombe la Dunia 2018.
“Nilizungumza na Zlatan Ibrahimovic siku ya Jumanne kuhusu kumshawishi kufuta maamuzi yake kustaafu na kurudi kwa ajili ya Kombe la dunia lakini amesema hajafuta uamuzi wake wa kustaafu, hawezi kurudi timu ya taifa”>>> Lars Richt
Maamuzi hayo ya Zlatan yamewashangaza wengi maana siku chache zilizopita Zlatan kupitia mahojiano aliyofanya na CCN alitoa kauli kuwa atashiriki Kombe la dunia 2018 baada ya kuulizwa na kusema “Kombe la dunia bila Zlatan haliwezi kuwa Kombe la dunia” Zlatan kwa sasa anaichezea club ya LA Galaxy ya Marekani
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao