Aliyekuwa Mhasibu wa Manispaa ya Moshi Richard Mfugale, Afisa utumishi Marrystela Massawe, Musa Musa Afisa manunuzi pamoja na Leticia Katalaiya mpiga chapa wa manispaa hiyo wamefikishwa mahakamani kwa kosa la Uhujumu Uchumi nakujipatia Milioni 58
Watuhumiwa hao wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Moshi na TAKUKURU Mkoani Kilimanjaro mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Sophia Masati
Watuhumiwa hao wanadaiwa kudanganya kuingia mkataba na Halmashauri ya Moshi kutoa magari 100 kutoka kwa kampuni ya Mshasha Royal Trans kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 nakujipatia zaidi ya Milioni 58.
Watuhumiwa hao kwa pamoja wameachiwa kwa fungu la dhamana la Shilingi Milioni thelathini huku upelelezi ukiwa umekamilika.