Mtanzania Abdi Banda anayecheza soka la kulipwa katika club ya Baroka FC ya Afrika Kusini amefanikiwa kuvaa medali ya Ubingwa wa kwanza toka amejiunga na timu, kufuatia ushindi wa fainali ya michuano ya Telkom Cup kwa kuifunga Orlando Pirates kwa mikwaju ya penati.
Baroka FC ambayo iliingia fainali ya michuano hiyo dhidi ya Orlando Pirates ilifanikiwa kuibuka Mabingwa kwa mikwaju ya penati 3-2, hiyo ni baada ya game kumalizika wamkiwa wamefungana sare ya magoli 2-2, Banda akiwa sehemu ya kikosi hicho kilichotwaa Ubingwa huo na kuweka historia katika maisha yake ya soka la kulipwa.
“Kwa napenda kumshukuru mwenyeji Mungu unajua huku kuna Makombe kama matatu, kuna hili Kombe la Ligi Kuu, Kombe la Telkom na Kombe la NedBank, sasa sisi tumechukua Kombe la Telkom Cup na tulicheza fainali Jumamosi, tukamfunga Orlando Pirates tulitoka 2-2 ila tukamfunga kwenye penati 3-2”>>> Abdi Banda
Hii inakuwa ni sehemu ya mafanikio kwa Abdi Banda ambaye licha ya ugeni katika kikosi hicho, amekuwa na wakati mzuri na mchezaji tegemeo kiasi cha kufikia hatua ya kupewa unahodha msaidizi katika timu, Banda ni miongoni mwa mabeki bora wanaotegemewa katika timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe