Bilionea anayemiliki kampuni ya Mohammed Enterprises nchini (MeTL), Mohammed Dewji `Mo’ ametoa ujumbe kuelekea mwaka 2018 na kuwataka vijana na Watanzania kiujumla kuacha kulalamika mwaka 2018.
Dewji katika ujumbe wake alioutoa kupitia mitandao yake ya kijamii ya Facebook, Instagram amewasihi Watanzania kama wanaona hawapendezwi na kitu fulani njia nzuri ni kukibadili kitu hicho na kuacha kulalamika kwani hakutaweza kubadili jambo lolote lile.
“Kama hupendi kitu fulani, (jaribu) kibadilishe! Unataka kupunguza uzito? Badilisha milo yako, fanya mazoezi. Unataka kukutana na watu wapya? Toka nje, tembea na jichanganye na watu wengine! Kumbuka kulalamika hakubadilishi jambo usilolipenda!” – Dewji
LIST KAMILI YA WANAOSHINDANIA TUZO YA VIJANA 50 WA KITANZANIA WENYE USHAWISHI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA