Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET) ipo kwenye maandalizi ya Kongamano la 32 la Kitaifa (National Conference) ambalo linaandaliwa kwa kushirikiana na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) na Chama cha waandisi washauri Tanzania (ACET).
Kongamano hili litafanyika tarehe 30 Novemba mpaka tarehe 2 Disemba 2023 katika Ukumbi wa Kimataita Arusha (AICC), jijini Arusha.
Taasisi inatekeleza majukumu yake kwa kupitia matawi yake yaliyopo katika mikoa takribani 16 nchini.
Taasisi ina malengo ya kufungua matawi katika mikoa yote nchini ili kuongeza wigo wa ushiriki wa Wahandisi katika kutekeleza dira na dhamira ya Taasisi. Vile vile, IT inafanya shughuli zake kwa kushirikina kwa karibu zaidi na mamlaka ningine zinazodhibiti/zene mtazamo wa kuendeleza shughuli za kihandisi, zikiwemo:
Taasisi ya wahandisi Tanzania (IET) ilianzishwa kwa kusajiliwa kama Asasi isiyo ya kiserikali mwaka 1975 chini ya Sheria ya Kusajili Vyama visivyo vya kisiasa
“Societies Act, 1954” na kama chama cha kitaaluma, kwa madhumuni ya kukuza tani ya uhandisi, sayansi na teknolojia nchini; na dhamira ikiwa ni kuhakikisha ubora/ufanisi wa kazi za kiuhandisi (Engineering Excellence) chini na nje ya mipaka ya chi.
Katika kufanikisha madhumuni a dhamira tajwa, na kwa kufuata Katiba ya Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), majukumu mojawapo ya taasisi hii ni pamoja na: Kutoa mafunzo ya muda mfupi kupitia mikutano, semina, makongamano na warsha zene maudhui va uhandisi ili si tu kwa madhumuni ya kuwaiengea uwezo wanachama wetu ili waweze kukabiliana na changamoto za kihandisi mahala pa kazi; bali pia kutengeneza nafasi/majukwaa kwa Wahandisi na Mafundi kukutana, kujadili na kutathimini utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi na changamoto zilizopo na kutafuta suluhisho kwa njia sahihi; na kuishauri Serikali kuweka msisitizo wa mendelezo wa masuala ya uhandisi na wahandisi kwa jumla il kuongeza tija katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kiuhandisi na kufikia maendeleo endelevu ya seta mbalimbali za kiuchumi na nchi yetu kwa ujumla.
Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET) inafanya majukumu yake kwa kutumia kamati za Baraza la Taasisi ama za kiutendaji; Vitengo vya Taasisi: Kitengo cha Wahandisi Wanawake (Women Chapter), Kitengo cha Wahandisi Wanajeshi (Military Chapter), Kitengo cha Wanafunzi (Students Chapter) a Kitengo cha Mafundi (Technicians Chapter).