January 16, 2019 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za tukio la shambulizi linalohusishwa na ugaidi, lililofanyika kwenye eneo lenye shughuli mbalimbali za kijamii, katika Hoteli ya DusitD2, Nairobi, nchini Kenya, siku ya Jumanne, January 15, mwaka huu.
Nanukuu taarifa ya CHADEMA “Kipekee CHADEMA inatuma salaam za pole kwa watu wote walioathiriwa na tukio hilo, kwa kupoteza maisha ya wapendwa wao na wengine waliojeruhiwa. Tunawatakia majeruhi wote uponaji wa haraka”
TUKIO LA UGAIDI KENYA: RAIS MAGUFULI NA KENYATTA WAMEZUNGUMZA