Baada ya staa wa Argentina Lionel Messi kubainika kuwa anajiunga na Club ya Inter Miami ya Marekani na sio FC Barcelona kama ilivyokuwa inazaniwa na wengi hapo awali.
Club ya Barcelona imetoa msimamo wake kuhusiana na kilichotokea dakika za mwishoni kuhusu Lionel Messi kubadili maamuzi na kwenda Inter Miami.
“Jumatatu ya Juni 5 Jorge Messi ambaye ni baba na muwakilishi wa mchezaji huyo, alimtaarifu Rais wa Club Joan Laporta kuwa maamuzi ya mchezaji (Messi) ni kujiunga na Inter Miami”
“Licha ya kuwa Barcelona walipeleka proposal yenye nia kwa pande zote mbili Barcelona na Messi kuvaa tena jezi zao, Rais Laporta anaelewa na kuheshimu maamuzi ya Messi, FC Barcelona inamtakia kila la kheri katika ukurasa mpya wa maisha yake ya soka”
Messi alijiunga na Barcelona toka 2000-2003 timu za vijana na baadae 2003 akaanza kucheza timu C, B na timu za wakubwa hadi alipoondoka 2021 na kujiunga na PSG.