Jeshi la Polis mkoa wa dodoma linamshikilia Raphael Keneth Ndamahnwa mlinzi wa kanisa Katoliki parokia ya watakatifu wote lililopo Nzuguni B kwaajili ya uchunguzi wa kifo cha msanii wa muziki wa kizazi kipya Joseph Francis Maarufu kama ManDojo kilochotokea agost 11 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa dodoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi SACP Anania Amo ambaye amesema jeshi la polisi linaendelea kumuhoji Raphael Keneth kuhusiana na Tukio hilo huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwaajili ya chunguzi na madaktari ili kubaini chanzo cha kifo chake.