Taasisi ya Kilimo hai nchini (TOAM) imepanga kuzindua mkakati wa kilimo hai wenye kuhimiza umuhimu wa kutunza asili Kwa ajili ya Afya naazingira Kwa ujumla.
Aidha imeomba serikali kutenga sehemu ya Fedha Kwa ajili ya Kilimo hai hata katika miradi mbalimbali ya Kilimo inayoendelea nchini ukiwemo ule wa kuwezesha Vijana katika kilimo ( BBT).
Mtendaji Mkuu wa TOAM, Bakari Mongo alisema hayo Jana Dar es Salaam wakati akizungumzia mkutano wa tatu wa kitaifa wa kilimo hai (NEOAC) unaotarajiwa kufanyika Novemba 8_9,2023 mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa TOAM ambaye Pia ni Mjumbe wa Kamati ya kumshauri raisi katika masuala ya uhakika wa chakula Mwantima juma amesema wanazungumza na wizara ya kilimo katika sehemu zinazogawiwa kama kuna watu watakubali kulima kilimo hai waruhusiwe kwani inawezekana ikawa fursa nzuri ya kuona unafuu wa gaharama, faida na soko kuhusiana na BBT.