Taasisi isiyo ya kiserikali ya LALJI FOUNDATION imetoa msaada wa vifaa pamoja na sare za shule kwa kwa watoto yatima 400 kutoka vituo mbalimbali vya kulea watoto yatima jijini Dar es salaam lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha utoaji wa elimu bora nchini.
Akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa vifaa hivyo Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mhe. Faustine Ndugulile ameipongeza taasisi hiyo kwa kuendelea kugusa makundi mbalimbali katika jamii huku akiwataka watoto hao kutumia fursa hiyo kuongeza juhudi katika kusoma ili kuongeza ufaulu wao na hivyo kuchangia katika maendeleo endelevu ya jamii
“Hongereni sana Lalji Foundation kwa jambo hili. Tukio hili ni la muhimu sana. Na kwa watoto rai yangu ni moja, tumewezeshwa tusome, na tuwe na tabia nzuri”, Mhe. Faustine Ndugulile
Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Walid Omar amesisitiza umuhimu wa kurudisha kwa jamii huku akiipongeza familia ya Lalji kwa kugusa kundi hilo la muhimu katika jamii.
Kwa upande wake Ndugu Mohsin Lalji ambae ni Mlezi wa LALJI FOUNDATION na Kiongozi wa familia ya Lalji amesema familia wameanzisha taasisi hiyo ili kusaidia jamii.