Taasisi ya mtetezi wa Mama imepinga vikali maandamano yanayoratibiwa na chama Cha demokrasia na maendeleo chadema kwa kusema chama hicho kimekosa hoja za msingi katika kuelekea kwenye chaguzi mbalimbali.
Mwinyi Idd Ludete ni mwenyekiti wa hamasa taifa mtetezi wa mama akiongea na waandishi wa habari katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Saalam akiwa na viongozi wenzake mbalimbali Amesema Rais Samia amefanya mengi makubwa kwa taifa la Tanzania hivyo anapaswa kuungwa mkono kwa ukubwa zaidi ili taifa lipate maendeleo zaidi.
Aidha Mwinyi Ludete amesema wao wanamuunga mkono Rais Samia kwani ni kiongozi ambaye ameleta mageuzi makubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo kwenye Afya, Elimu,na miundombinu mingine mbalimbali huku watalii wakizidi kuongezeka kutokana na Amani iliyopo.
Mwenyekiti wa Hamasa Taifa Mwinyi Amesisitiza maandamano yasio na ridhaa ya serikali ni kuvunja sheria hivyo amewataka chadema kutumia njia nyingine ya amani nasio maandamano ambayo mengi usababisha uvunjifu wa amani.