Taasisi Za dini nchini Zimetajwa Kuwa Chachu ya Mabadiliko Chanya Ikiwemo Kukemea Mmomonyoko Wa Maadili kwa jamii pamoja na vitendo vya Rushwa.
Kauli Hiyo Imetolewa na Mbunge Viti Maalum Kundi la Vyuo Vikuu Tanzania Dr Paulina Nahato katika Ibada maalum ya harambee ya ujenzi wa Jengo la makao Makuu ya Kanisa la waadventista wa sabato Lililopo Wilaya Ya Babati Mkoa wa Manyara ambalo mpaka kukamilika kwake litagharimu shilingi Bilion 1.3.
“Namshukuru Sana Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa na Wabunge wenzangu wametoa mchango mkubwa sana katika kujitoa kwenye umaliziaji wa jengo hili,taasisi za dini zimekuwa mbele katika kukosoa na kukemea matendo maovu ili kuleta mabadiliko chanya katika Taifa letu”
Kwa Upande Wake Askofu wa Kanisa hilo Dr David Mpwani amesema Kanisa Hilo limejikita kutoa Elimu kwa jamii ili kupata uelewa wa mambo mbalimbali, na kukemea Vikali Vitendo vya Rushwa na mmomonyoko wa Maadili.
“Serikali yetu inatambua umuhimu wa taasisi za dini na ndio maana tunaomba wakitusapoti kwa kiasi kikubwa,sisi kama kanisa tunapinga vikali matendo yote yasiyoendana na Maadili ya kitanzania kama maandiko yanavyosema”