Taasisi mbalimbali za kiraia zinatarajia kukutana jijini Arusha kwa kujadili na kutatua changamoto mbalimbali zinazoathiri mifumo ya techenolojia kwa lengo la kuimarisha na kuboresha SEKTA hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa kituo cha sheria na Haki za binadamu Dkt Anna Henga amesema changamoto inayowaathiri wananchi ni pamoja na kukosekana kwa kwa mtandao hasa vijini na kukatika kwa umeme mara kwa mara.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya wiki Azaki Nesia Mahenge ameeleza mambo yatakayojadiliwa Katika mkutano huo.
Naye Mchambuzi wa kijinsia kutoka mtandao wa jinsia Deogratius temba amesema watahakikisha wanawake wanawezeshwa kutumia technojia bila kubagiliwa.