Chama cha Wataalamu wa Misitu Tanzania (TAF) kimeaswa kuanzisha hifadhi zake za misitu katika maeneo mbalimbali nchini ili kuepukana na changamoto ya ukosefu wa fedha za kuendesha chama.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula alipokuwa anafungua mkutano wa 20 wa mwaka wa kisayansi na mkutano mkuu wa 28 wa mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Misitu Tanzania (TAF) katika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAFORI) mkoani Morogoro.
Wataalamu wa misitu nchini wameaswa kulinda maadili ya taaluma yao kwa kuepuka vitendo vya rushwa kwa kuwa kuna baadhi ya wataalamu wamekuwa wakijihusisha na vitendo hivyo ambavyo vinavunja misingi na taratibu za uhifadhi wa misitu nchini.
Mhe. Kitandula alisema kuwa wataalamu wa misitu wanatakiwa kuendelea kuimarisha mandhari na mifumo ikolojia ambayo imeharibiwa hasa vyazo vya maji, wakitambua kwamba maji ndiyo tegemeo kubwa kwenye miradi mbalimbali ya Serikali ukiwemo Mradi mkubwa wa Umeme wa Maji wa Julius Nyerere kule Rufiji.
Alisisitiza kuwa wanatakiwa kutoa mafunzo, kuhamasisha na kujenga ufahamu wa kutosha kwa jamii juu ya faida na thamani ya miti na mifumo ikolojia inavyofanya kazi.
Vilevile alisema kuwa Serikali, kwa nafasi yake imekuwa ikichukua hatua stahiki za kuhakikisha nidhamu inakuwepo miongoni mwa Wataalamu wa misitu walioajiriwa na Serikali ili kuboresha usimamizi endelevu wa misitu.
Akitolea mfano katika hatua kubwa ambayo Serikali imechukua katika kuweka nidhamu na maadili ni kubadili mfumo wa