“Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania imetoa angalizo la mvua kubwa leo April 29 2021 katika maeneo ya Tanga na Visiwa vya Unguja na Pemba”
“Athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na baadhi ya makazi ya Watu kuzungukwa na maji na kuchelewa kwa shughuli za usafiri na usafirishaji, Wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari na kuendelea kufatilia taarifa za hali ya hewa” — Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania imetoa tahadhari hii siku chache tu baada ya kutoa tahadhari nyingine ya kimbunga kiitwacho ‘jobo’ ambacho kilitarajiwa kutokea Tanzania lakini hata hivyo siku chache baadae Mamlaka hiyo ilitangaza kwamba kimefifia nguvu na kikaishia baharini bila kufika Nchi kavu.
Leo April 29 2021 imenyesha mvua katika maeneo mbalimbali ikiwemo Dar es salaam na hadi sasa hakuna ripoti yoyote ya madhara, tunaendelea kukaa karibu na Mamlaka mbalimbali za Serikali ili kukufahamisha habari zote juu ya mvua hizi.