Mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga ambayo ilichezwa April 19 imeingia kwenye headline baada ya kuhusishwa na imani za kishirikina na hii ni baada ya kufukuliwa kwa mayai 3 uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Urio ambaye ni Meneja wa Uwanja wa taifa amepatikana kulizungumzia hili ameanza kwa kusema>>’Unajua mambo yanayohusiana na mambo ya kishirikina kwanza Serikali haiyaamini,wanaozungumza mambo ya kishirikina siwezi kuwakataza kuzungumza kwa sababu kila mtu ana imani yake lakini sisi vitu hivyo hatujihusishi,hatuvutaki na hatutojihusisha nayo kabisa kwa sababu hayako kwenye imani zetu na sio sehemu ya kazi’
‘Ni uongo kabisa vitu vifukuliwe uwanjani kama waliona na kama mtu aliingia nalo yai huwezi kumwambia mtu hakukaguliwa kwa sababu yai hata ukipita kwenye vile ving’amuzi vya polisi haviwezi kung’amua kwa sababu yai sio chuma hivyo haviwezi kupiga kelele lakini hiyo mimi siwezi kuelezea kwa sababu sijasikia mambo ya mayai wala kusikia sijaona vitu vya uchawi lakini nimesikia watu wanazungumza’
‘Hii ipo kwenye michezo yote unayaikia ooh wameroga hawa wamefanya hivi na huwezi kuwazuia watu kusema kwenye uwanja mpya wa Taifa haijawahi kutokea’.