Headlines za soka la bongo bado zinauzito wake hususani kuhusiana na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ambayo November 14 ilicheza mechi yake ya kwanza ya kuwania kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2018 Urusi dhidi ya timu ya taifa ya Algeria, mchezo ambao ulichezwa uwanja wa Taifa Dar Es Salaam na kumalizika kwa sare ya goli 2-2.
Siku tatu baadae yaani November 17 ulichezwa mchezo wa marudiano mjini Blida Algeria katika uwanja wa Mustapha Tshaker, mchezo ambao ulimalizika kwa Taifa Stars kukubali kipigo cha kihistoria cha goli 7-0 na safari ya Kombe la Dunia kuishia hapo, kabla ya mchezo wa pili wa marudiano kamati ya ushindi ya Taifa Stars ilitangaza kuwa kama timu itaifunga Algeria mjini Blida basi itawapa wachezaji milioni 500.
Najua mtu wangu wa nguvu unataka kujua zile milioni 500 zimeenda wapi? ni zile za michango? au, November 26 majibu yake yameifikia millardayo.com, kupitia makamu mwenyekiti wa kamati ya ushindi ya Taifa Stars Michael Richard Wambura ametoa mchanganuo wa fedha hizo, sambamba na kufikia makubaliano na Rais wa TFF Jamal Malinzi kuvunja kamati hiyo.
“Tulipokea michango kutoka kwa watanzania ambayo inafikia milioni 122, baada ya mchezo wa Dar kamati iliahidi kutoa milioni 500 kwa wachezaji kama wataifunga Algeria kwao, zile milioni 500 hazikuwa mikononi mwa kamati bali ni watu ambao walikuwa wameahidi kutoa kama timu ingeshinda, kwa hiyo kwa ujumla wake kama wangetoa ndio hizo pesa zingefikia milioni 500, hiyo ilikuwa ahadi kama tungeshinda zingetolewa” >>> Michael Wambura
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.