Baada ya Marekani kuripotiwa kukumbwa na baridi kali hali iliyopelekea baadhi ya viwanja vya ndege, Barabara na reli kufungwa kwa muda..headlines zimehamia Taiwan.
Wakati Tanzania ikikadiriwa kuwa na nyuzi 38°C na kuendelea kwa sasa, unaambiwa mji wa Taipei uliopo Taiwan umekumbwa na baridi kali huku nyuzi joto ikiwa ni 4°C, joto ambalo ni dogo na halijawahi kutokea kwa miaka 44 iliyopita.
Mpaka sasa tayari watu 52 wamepoteza maisha kutokana na kushindwa kuhimili baridi kali…wengi wao wakiwa wameugua nimonia pamoja na maradhi ya moyo.
Watalii zaidi ya 60,000 pia wamekwama Korea Kusini kutokana na baridi kali, pia safari za ndege zimesimama kwa muda.
Miji mingine iliyoathirika ni Hong Kong na Japan.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.