Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Kilimanjaro kupitia kwa Kamanda Holle Makungu imemfikisha Mahakamani aliyekuwa Afisa Uchaguzi mwaka 2015 katika jimbo la uchaguzi Siha Stanry Kopola ambaye pia ni mwanasheria.
Mtuhumiwa huyo anakabiliwa na shtaka la uhujumu uchumi wa jumla ya zaidi ya milion 7 na anakabiliwa na makosa 14. Makungu amesema mtuhumiwa huyo alipokea fedha hizo na kuandaa nyaraka za udanganyifu na kumdanganya mwajiri.