Saa kadhaa baada ya kamati ya utendaji wa Yanga kupitia mjumbe wa kamati hiyo Salum Mkemi kutangaza kupinga rufaa ya Simba dhidi ya Kagera Sugar kwa kumtumia mchezaji Mohamed Fakih aliyedai kucheza dhidi ya Simba akiwa kaoneshwa kadi tatu za njano, Simba kupitia afisa habari wao Haji Manara wametoa taarifa kwa vyombo vya habari.
Yanga walisema mchezaji Fakhi anayekatiwa rufaa amekubali kuwa ana kadi tatu za njano lakini mbili za VPL na moja ni kadi ya FA hivyo hazihusiani na ilikuwa halali kucheza katika mchezo dhidi Simba, Yanga wanahisi Simba wanafanya udanganyifu ili wapate point za mezani na kuitoa Yanga kileleni.
11-4-2017. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Leo mchana huu kunatembea taarifa iliyotolewa na klabu ya Yanga inayoonyesha kuishinikiza Bodi ya ligi kutokutenda haki juu ya rufani yetu dhidi ya klabu ya Kagera Sugar kwa kumchezesha mchezaji Mohammed Fakih aliyecheza dhidi yetu akiwa na kadi tatu za njano ambalo ni kosa kisheria.
Taarifa hiyo ya Yanga iliyomnukuu Mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo Salum Mkemi aliyeongea mbele ya waandishi huku akiwa na katibu mkuu wa klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa iliitaka bodi kutokutoa points kwa Simba eti kwa kuwa hizo points zitawaathiri Yanga kwenye kutetea ubingwa wao ambao kwa sasa upo rehani.
Taarifa hiyo imeonyesha Yanga wanao ushahidi kuwa Fakih ana kadi mbili za njano.
Klabu ya Simba inawaambia viongozi wa Yanga wanayo mambo ya msingi ya kuwashughulisha, ikiwepo kutafuta mishahara ya wachezaji wao iliokwama kwa miezi kadhaa kama inavyoripotiwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari.
Waangalie namna bora ya kuurejeshea hadhi uwanja wake wa mazoezi wa Kaunda ili upate kuchezeka tena na sio ulivyo hivi sasa,ambapo umegeuka kama bwawa la kufugia kambale ni kushangazwa kulikochupa mpaka kufuatilia rufani isiyowahusu hii ni rufani ya Simba dhidi ya Kagera sio wao Yanga.
Tunaamini bodi haitafanya maamuzi kwa shinikizo la yoyote yule,na hatutarajii kuona porojo walizozisema leo zitaondoa ukweli uliopo mezani kwao ambao klabu yetu imeuwasilisha Mwisho niwaombe washabiki wetu watulie na waiachie bodi ifanye maamuzi yake ambayo tunaamini yatatoa haki kwa anayestahili.
IMETOLEWA NA.. Haji S Manara
Mkuu wa Habari wa Simba Sc
SIMBA NGUVU MOJA @simbasctanzania@mkemi1_supermarket
VIDEO: Simba imewafanya Yanga wapeleke taarifa TAKUKURU na TCRA