Kaburi la pamoja nje ya Damascus lilikuwa limezikiwa miili ya watu 100,000 waliouawa na utawala wa Rais aliyepinduliwa Bashar al-Assad, kulingana na mkuu wa Kikosi Kazi cha Dharura cha Syria.
Mouaz Moustafa alisema eneo la al-Qutayfah kilomita 40 kaskazini mwa mji mkuu wa Syria, ni moja ya makaburi matano ya halaiki ambayo ameyatambua kwa miaka mingi, kulingana na Reuters.
“Laki moja ndio makadirio yasasa” ya idadi ya miili iliyozikwa , alisema Moustafa.
“Ni makadirio makubwa sana, yasiyo ya haki.”
Moustafa alisema kuna makaburi zaidi ya halaiki ambayo, pamoja na wahanga wa Syria, na wageni.
Mamia ya maelfu ya Wasyria wanakadiriwa kuuawa tangu 2011 wakati ukandamizaji wa al-Assad dhidi ya maandamano dhidi ya utawala wake ulikua vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe.