Takriban wanajeshi 200 wa Ufaransa wameondoka katika mji wa Ouallam ulioko kusini-magharibi mwa Niger huku kukiwa na uondoaji mkubwa wa vikosi vya Ufaransa unaoendelea katika taifa hilo la Sahel, kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali cha Tele Sahel kinaripoti.
Ilisema kuwa wanajeshi 193 wa Ufaransa walioko Ouallam waliondoka kambi yao kuelekea Chad siku ya Jumapili.
Wanajeshi hao waliripotiwa kuondoka na lori 28 pamoja na magari 24 ya kivita na magari mengine ya msaada.
Chad ilikuwa imekubali kutoa “pengo ” la kuwaondoa wanajeshi wa Ufaransa kutoka Niger kurudi Ufaransa.Zoezi la kujiondoa lilianza tarehe 5 Oktoba.
Ufaransa ilituma wanajeshi 1,500 nchini Niger kusaidia kukabiliana na uasi unaozidi kuongezeka wa wanajihadi tangu 2015.
Wanajeshi hao wa Ufaransa walikuwa na makao yake katika mji mkuu Niamey, Ouallam na Ayorou – karibu na mpaka na Mali.